Tuesday, August 12, 2025

WABUNGE WA BUNGE LA TAIFA KOREA WATEMBELEA OFISI YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM


















Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 12, 2025 amewapokea  waheshimiwa wabunge wa Bunge la Taifa Korea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Waheshimishwa wabunge kutoka Bunge la Korea ambao wametembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kupata wasaa wa kufanya mazungumzo na Mhe Mkuu wa Mkoa ni Mhe Lee Jae Jung, Mhe Kim Hyung Dong, Mhe Boo Seung Chan na Mhe Lee Bang Woo.

Akiongea baada ya kuwapokea wageni hao ofisini kwake Ilala Boma  RC Chalamila amesema Mkoa unajivunia kuwa mwenyeji wa miradi mikubwa inayotokana na ushirikiano wa kirafiki kati ya mataifa yetu mawili aidha nipende kugusia baadhi ya miradi mikuu chini ya mfuko wa ushirikiano  wa maendeleo  ya kiuchumi  EDCF wa Korea pamoja na fursa mpya za ushirikiano zaidi kwa mfano ujenzi wa Hospitali ya Mloganzila, mradi ambao ulifadhiliwa na Benk ya Exim ya Korea kupitia mkopo nafuu, mradi wa daraja la Tanzanite, Kituo cha Taifa cha hifadhi ya Taarifa za Vitambulisho.

Vilevile Korea imekuwa ikifadhili sekta mbalimbali kama Ujenzi, Usafirishaji bandarini, Mazingira, Usimamizi wa taka, na ujenzi wa uwezo, pia makampuni kutoka Korea yamesaidia sana katika miradi ya DMDP,  Mfumo wa mabasi yaendayo haraka BRT, na madaraja makubwa.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam  Ndg Abdul Mhite amesema Mkoa huo umebarikiwa kuwa na fursa nyingi za kimaendeleo hivyo kwa niaba ya Serikali na wananchi anawakaribisha sana waheshimiwa wabunge kutoka Jamhuri ya Korea ambapo ameomba mashirikiano baina ya pande zote mbili yaendee  kudumu kwa masilahi mapana ya wananchi wa Tanzania na Korea.

Mwisho, Mhe Mkuu wa Mkoa amepongeza kwa utaalamu wao, uwekezaji wao na urafiki wa dhati, ambapo ametoa rai kuendeleza msingi huo wa ushirikiano ili kujenga maisha ya baadaye yaliyojaa ubunifu, ujumuishi, na manufaa ya pande zote mbili Tanzania na Korea.

No comments:

🔴🔴 TAWA YASAINI MIKATABA YA UWEKEZAJI MAHIRI YENYE THAMANI YA TZS BILIONI 719

📍 Neema yaja kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya uwekezaji 🖊️ Na Beatus Maganja, Dar es Salaam Katika hatua ya kihistoria na kishin...