
Ndugu Ussi ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Nyabisarye Mahakama kuu Kanda ya Musoma yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami .
Ussi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa lengo la kuwarahisishia wananchi huduma katika maeneno yao ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi na kujiingizia kipato.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Wilaya ya Musoma Mhandisi Mohamed Etanga amesema jumla ya shilingi Milioni 600.97 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Nyabisarye- Mahakama Kuu yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami .
Amebainisha kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulianza Oktoba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba, 2025.
Mhandisi Etanga ameongeza kusema kuwa barabara hiyo endapo itakamilika itakuwa kiunganishi cha Kata ya Bweri na Kata ya Rwamlimi na kuwa kiungo kikubwa kwa wananchi katika kupata mahitaji ya kijamii kwa wepesi
No comments:
Post a Comment