Friday, August 08, 2025

KAMISHNA BADRU AWATAKA ASKARI WA JESHI LA UHIFADHI NCAA KUZINGATIA WELEDI KATIKA KAZI.









Na Mwandishi wetu, Pololeti Ngorongoro 

Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-razaq Badru amewataka askari wa uhifadhi katika Pori la Akiba la Pololeti Wilayani Ngorongoro kuzingatia maadili, weledi na matokeo ya kazi wanazozifanya ili kulinda hadhi ya jeshi hilo.

Kamishna Badru ametoa rai hiyo alipokuwa katika ziara ya kikazi na kuzungumza na baadhi ya askari hao alipotembelea Pori la Akiba la Pololeti kukagua hali ya uhifadhi na ulinzi katika eneo hilo.

Aidha Kamishna Badru ameridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na askari hao hali iliyosababisha eneo hilo kwa sasa kuwa na idadi kubwa ya wanyama mbalimbali wakiwemo tembo, twiga, simba, swala, pofu, nyumbu, pundamilia na spishi nyingine za wanyama.

Badru amewahakikishia askari hao kuwa miundombinu mbalimbali ya eneo hilo itaboreshwa sambamba na kujengewa mazingira bora ya kufanyia kazi ili kuendelea kuboresha mazingira ya ulinzi na uhifadhi endelevu.

No comments:

MAPOKEZI YA KISHINDO KWA WAGOMBEA WA CCM JIJINI DODOMA!

                                                                                                          Dodoma, 09 Agosti 2025 — Umati m...