Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametembelea nyumbani kwa marehemu Mhe. Job Yustino Ndugai, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kilichopo Mtaa wa Njedengwa jijini Dodoma, kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo chake.
Akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Balozi Nchimbi alitoa pole kwa mjane wa marehemu, Dkt. Fatma Mganga, pamoja na familia na ndugu waombolezaji waliokusanyika nyumbani hapo leo Ijumaa, tarehe 9 Agosti 2025.
Katika ziara hiyo, Balozi Nchimbi pia alisaini kitabu cha maombolezo na kuungana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu, akieleza kuwa kifo cha Mhe. Ndugai kimeacha pengo kubwa katika uongozi na historia ya Bunge la Tanzania.
No comments:
Post a Comment