Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mzava, ameongoza kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Kupaanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mji.
Kikao hicho kimefanyika leo, Machi 12, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Geophrey Pinda, wakishirikiana na wataalamu mbalimbali kutoka wizara husika.
Lengo la kikao ni kupitia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo muhimu ambao unalenga kuweka mpangilio mzuri wa matumizi ya ardhi, kupunguza migogoro ya ardhi, na kuongeza kasi ya utoaji wa hatimiliki kwa wananchi wa Babati.
Mradi wa KKK unatajwa kuwa moja ya juhudi muhimu za serikali katika kusimamia rasilimali ardhi kwa ufanisi na kuhakikisha wananchi wanamiliki ardhi yao kwa mujibu wa sheria.
#KKK #ArdhiKwaMaendeleo 🌍 #Manyara 🚜 #MipangoMiji 📜
No comments:
Post a Comment