*Asisitiza kuwa mifugo ni uchumi, ajira na biashara
*Atoa wito kwa wakulima na wafugaji wawe wamoja
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuweka mikakati
madhubuti ya kuhakikisha sekta ya mifugo inakuwa endelevu na yenye tija.
Amesema
kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan mara zote ameweka msisitizo
katika kuiendeleza sekta hiyo kwa kuwa mifugo ni uchumi, ajira na ni
biashara.
Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipozungumza na
wananchi katika mikutano aliyoifanya jana Jumatano (Machi 12, 2025)
Wilayani Igunga, mkoani Tabora ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya
siku mbili.
“Tunawahamasisha wafugaji, fugeni mifugo ni uchumi,
mifugo ni maisha na mifugo ni pesa na wakulima limeni tupate mazao mengi
ya chakula na biashara na ni lazima wafugaji na wakulima tuelewane.”
Katika
hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini
kuweka mikakati ya kuhakikisha wanakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na
kuzisimamia fursa zilipo kwenye maeneo yao ili kuwanufaisha wananchi.
“Mkifanya hivyo mtakuwa mmewasaidia wananchi kujiendeleza kiuchumi.”
Akizungumza
baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye shule ya Sekondari ya Seif
Gulamali, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka jamii kuweka nguvu za pamoja
katika kumlinda mtoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao.
Pia,
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia
utekelezaji wa mikakati iliyopo katika sekta ya elimu ili sekta hiyo
iweze kuwanufaisha watanzania kwa kukuza ubora wa elimu nchini.
Thursday, March 13, 2025
MAJALIWA: SERIKALI ITAENDELEZA MIKAKATI YA KUKUZA SEKTA YA MIFUGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA SADC KWA NJIA YA MTANDAO
Dodoma, 13 Machi 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, ...

-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
(Picha na Yahya Charahani) Kwa wale waliokulia maeneo haya, hili ni jambo la kawaida ukitoka mjini, shambani sijui hadi wapi kote ni haya h...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
No comments:
Post a Comment