Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya akizungumza leo na Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 wakati wa mafunzo ya wakufunzi hao yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro. Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Mtalaamu wa Kilimo na Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Zanzibar Mzee M. Mzee akiwafundisha Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya wakufunzi hao yanafanyika mkoani Morogoro ambapo utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Mmoja wa Wakufunzi akiuliza swali wakati wa mafunzo ya Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 yanayofanyika mkoani Morogoro. Utafiti huo wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Baadhi ya Wakufunzi wakijifunza mbinu mbalimbali zitazotumika kuwafundishia Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya wakufunzi hao yanafanyika mkoani Morogoro ambapo utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akitoa maelekezo kwa waratibu wa mafunzo ya Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya Wakufunzi hao yanafanyika mkoani Morogoro na utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
Na: Veronica Kazimoto-Mororgoro.
Jumla ya wakufunzi 52 wakiwemo Mameneja Takwimu wa mikoa yote nchini wamepewa mafunzo juu ya mbinu mbalimbali zinazotumika kufundishia wadadisi kwa ajili ya kupata takwimu bora za kilimo na mifugo.
Mafunzo hayo ya wiki moja yanayoendelea kufanyika mkoani morogoro, yanalenga kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili waweze kuwafundisha wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa Mwaka 2017 kwa ajili ya kupata takwimu rasmi zitakazotumika katika kupanga mipango ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amewataka wakufunzi wao kuzingatia kwa makini mafunzo hayo ili waweze kuwafundisha kwa ufanisi wadadisi wakaokusanya taarifa za utafiti huo wa kilimo na mifugo.
"Ili kuiwezesha nchi yetu kupata takwimu bora za kilimo na mifugo inatakiwa ninyi wakufunzi kuzingatia kwa makini mafunzo haya ili muweze kuwafundisha kwa ufanisi mkubwa wadadisi ambao watazunguka nchi nzima kukusanya takwimu za kilimo na mifugo", amesema Ruyobya.
Utafiti wa Kilimo na Mifugo hufanyika kila mwaka ambapo utafiti wa mwaka huu utafanyika kuanzia mwezi Oktoba, 2017 chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda na Biashara.
No comments:
Post a Comment