Friday, August 18, 2017

ULEGA AZINDUA MADARASA YALIYOJENGWA KWA USHIRIKIANO NA FAMILIA YA GHULAM HUSSEIN

Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akizindua madarasa yaliyojengwa kwa ushirikiano na familia ya Ghulam Hussein pamoja na mdau wa maendeleo na balozi wa heshima kutoka visiwa vya Seychelles Maria Van Pool (aliyevaa nguo nyekundu).

 Mbunge wa Mkuranga  Abdallah Ulega amefanikiwa kuzindua madarasa mawili katika shule ya msingi Muongozo kijiji cha Mwarusembe yaliyojengwa kwa hisani ya familia ya Ghulam Hussein ikiwa ni kuitikia ombi la Mbunge la kushirikiana na wadau mbalimbali katika  kuijenga Mkuranga.

Familia hii imeunganishwa na mdau wa maendeleo na balozi wa heshima kutoka visiwa vya Seychelles Maria Van Pool na Katika uzinduzi huo  Ulega aliwasisitiza wazazi kusimamia vyema maendeleo ya elimu ya watoto kwa kushirikiana na walimu.

Mbunge Ulega alisisitiza pia kutunzwa kwa miundombinu ya elimu ili iweze kudumu kwa mda mrefu na kuwanufaisha waTanzania walio wengi                       
  Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi katika hafla ya uzinduzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Muongozo kijiji cha Mwarusembe, Madarasa hayo yamejengwa kwa hisani ya familia ya Ghulam Hussein.                        
Muonekano wa nje wa madarasa hayo, pamoja na Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akiwa pamoja na  familia ya Ghulam Hussein pamoja na mdau wa maendeleo na balozi wa heshima kutoka visiwa vya Seychelles Maria Van Pool na wanafunzi wa shule wakiwa wamekaa katika madawati ndani ya madarasa hayo.
 Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akisalimiana na wazazi na  wanafunzi  katika hafla ya uzinduzi wa madara mawili katika shule ya msingi Muongozo kijiji cha Mwarusembe, Madarasa hayo yamejengwa kwa hisani ya familia ya Ghulam Hussein

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...