Wednesday, August 02, 2017

VETA NA AIRTEL YATHIBITISHA KUHUDUMIA WANAOTAKA KUJIFUNZA UFUNDI WALIKO

 Afisa Matukio wa Airtel Tanzania akikabidhi simu maalum zitakazotumika kuendesha mradi wa VSOMO kwa Msajili Mkuu Veta Kipawa(Registry), Bw,   Harold Mganga, (kushoto), akishuhudiwa na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi. (Project and Short Course Coordinator)Veta Kipawa Gosbert Kakiziba (katikati) simu hizo zimetolewa kwa  kwaajili  ya mradi wa VSOMO. VSOMO ni applikesheni maalum inayotoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.
Afisa Matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kulia) akimuonyesha applikesheni ya VSOMO  Mkuu wa Usajili Veta Kipawa (Registry) Bw,   Harold Mganga  (katikati) pamoja na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi. (Project and Short Course Coordinator) Veta Kipaw bw, Gosbert Kakiziba (kulia).  hafla fupi ya makabidhiano ya simu hizo yaliyofanyika  Veta Kipawa. Aplikesheni ya VSOMO inatoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.

Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kupitia mfumo wa mafunzo kwa mtandao wa VSOMO unaodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imebainisha kuwa iko tayari kuhudumia vikundi au jamii ya wanaotaka kujifunza ufundi stadi kwa kupeleka timu yao ya mafunzo kwa vitendo popote ili kuhakikisha dhana ya uchumi wa viwanda inakamilika kwa kuwa na mafundi wazuri waliohitimu ufundi katika chuo maalumu nchini

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha veta kipawa ambae pia ni msimamizi wa mradi wa mafunzo kwa njia ya simu unaodhaminiwa a Airtel kwa lengo la kutoa FURSA kwa vijana wegi mjini kupata ujuzi na kujiajiri Mhandisi Lucius Luteganya.

VETA tuko tayari kuwafuata wanafunzi wetu endapo watajiandikisha na kuhamasihana kwa kikundi kusoma kwa njia ya mtandao wa VSOMO , ikiwa watakuwa vijana kuanzia 15-20 na wakipenda kupata mafunzo waliko basi sisi tutawafuata waliko ili kuhakikisha wanahudumiwa na mobile trainers wetu”

“sasa hivi kupitia mtandao wa Vsomo tunakozi 12, wanafunzi wanaweza wakajisomea wawapo popote mara baada ya kupakua App yetu ya VSOMO na kulipia kozi anayotaka” alisisitiza Luteganya.

Eng Luteganja alitaja kozi hizo kuwa ni “Tunampango waongeza kozi zingine 15 hivi karibuni lakini kwa sasa zilizopo tayari kwenye mtandao ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani , Umeme wa magari, Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

Tangu VETA na Airtel walipozindua mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao waVSOMO mwezi wa Juni 2016 Mfumo huu wa VSOMO sasani umepata umaarufu mkubwa kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wameshasoma kozi mbalimbali na kupata vyeti vyao vya ufundi stadi kutoka VETA.

kujiandikisha katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO mwanafunzi atalipia kwa simu yake gharama ndogo ya shilingi 120,000 tu kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60#. na kufanya malipo ambazo gharama hizi zitamuwezesha kuja kupata mafunzo kwa vitendo bila malipo ya ziada.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...