Wednesday, August 16, 2017

NAIBU WAZIRI MHANDISI NGONYANI ATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA, AZUNGUMZA NA UONGOZI, WAFANYAKAZI WA SHIRIKA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati alipotembelea vitengo mbalimbali vya shirika hilo, kuongoea na Uongozi pamoja na wafanyakazi, Dar es Salaam. Wa tatu ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo kuhusu utendaji kazi wa kitengo cha utumaji na upokeaji wa fedha cha Western Union, katika ziara hiyo. 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo (kulia), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani kuhusu idara mbalimbali za Posta Kuu, wakati alipotembelea sehemu hiyo katika ziara hiyo. Kushoto ni Meneja wa Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto kwake), kuzungumza na Uongozi wa shirika hilo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa shirika, Hassan Mwang'ombe.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akizungumza nao katika ziara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta katika ziara hiyo. Kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirikahilo, Macrice Mbodo, kushoto ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde na kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa shirika, Hassan Mwang'ombe.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es Salaam.    
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta katika ziara hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakisikiliza na kuchukua habari, wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alipokuwa akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto kwake), mara baada ya kumaliza kuzungumza na Uongozi wa shirika hilo, katika ziara hiyo. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano wao na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipofika kwenye taasisi hiyo, kukagua sehemu mbalimbali za shirika, kuzungumza na Uongozi pamoja na wafanyakazi.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), kuzungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa ziara hiyo. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakati alipowataka kueleza matatizo yao yanayowakabili katika kazi zao kwenye shirika hilo. 
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Joyce Kagose akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, matatizo mbalimbali yanayowakabili kama wafanyakazi pia ya shirika hilo katika kujikwamua kimaendeleo.  
Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, akisikiliza kero za wafanyakazi wakati wa mkutano huo. 
Mfanyakazi wa shirika hilo, Ahmed Kaumo akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, matatizo yanayowakabili pamoja na yanayolikabili shirika kwa jumla.  
Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, akitaka ufafanuzi wakati mmoja wa wafanyakazi alipokuwa akielezea matatizo yanayowakabili katika kazi zao za kila siku kwenye shirika hilo. 
Mfanyakazi Jasson Kalile akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, jinsi shirika hilo, linavyokabiliwa na matatizo mbalimbali yanayolikwamisha kupiga hatu za haraka za kimaendeleo.
Zainab Matollah, mfanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, matatizo mbalimbali yanayowakabili katika kazi zao. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na wafanyakazi mara baada ya kusikiliza matatizo yao yanayowakabili katika utendaji wao wa kazi kwenye shirika hilo, la Posta.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na wafanyakazi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akisalimiana na kuagana na wafanyakazi mara baada ya kumaliza kuzungumza nao,  jijini Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...