Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Steve Kimea wa ZOLA akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo ambalo watakuwa wanatoa huduma pamoja na kuuza vifaa mbalimbali vitakavyotumika kupata umeme wa ZOLA.
DUKA jipya linalouza vifaa na kutoa huduma za umeme wa ZOLA lazinduliwa Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Akizungumza wakati uzinduzi wa Duka hilo Mkuu wa Kitengo cha Biasharawa ZOLA, Steve Kimea ametoa wito kwa Taasisi za Serikali ambazo hazina huduma za umeme hasa vijijini kushirikiana nao ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa kwenye vituo vya afya ili kuwasaidia wagojwa pamoja na kinamama wajawazito.
Amesema kuwa kampuni hiyo inayotoa umeme wa ZOLA hapa nchini imeshatoa huduma hiyo kwenye vituo vya Polisi pamoja na vituo vya huduma za afya na umeme upo vizuri.
Hata hivyo amesema kuwa utakapo nunua mtambo wa umeme wa ZOLA utatengenezewa mfumo wa umeme katika nyumba yako kwa bei nafuu na wengine kwani huduma zao zinalingana na maisha ya Mtanzania.
Amesema kuwa umeme wa ZOLA unaweza kutumika katika vifaa mbalimbali kama kuchaji simu, mashine za kunyolea, televisheni pamoja na kuwasha taa sita za ndani.
Pia ukinunua vifaa vya ZOLA utapata dhamana(Warrant) ya miaka mitano endapo kifaa chochote kitaharibika mteja utatengenezewa bila gharama yeyote ile.
Katikati ni Meneja Masoko wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akikata utepe kuzindua Duka linalouza na kutoa huduma za ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Mkuu wa kitengo cha mauzo wa ZOLA, John Amach na Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea wakishrikiana kukata utepe kuzindua duka hilo.
Duka la ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akipata maelekezo na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimealeo katika uzinduzi wa Duka jipya ambalo linatoa huduma mbalimbali za umeme wa ZOLA jijini Dar es Salaam leo.
Mfanyakazi wa kampuni inayotoa huduma ya umeme wa ZOLA akitoa maelekezo kwa baadhi ya wateja waliofika dukani hapo Mwenge jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindu wa duka hilo.
No comments:
Post a Comment