Sunday, March 19, 2017

KAYOMBO AKAGUA UKARABATI WA BARABARA YA SIMU 2000


Trekta ambalo linafanya kazi ya kukarabari barabara ya Simu 2000
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua barabara ya simu 2000 ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielekeza jambo kuhusu ukarabati wa barabara hiyo, Wengine ni Meneja wa stendi ya Simu 2000 Bakari Shehoza na Injinia wa Ujenzi katika Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga
MD Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo
Barabara inayofanyiwa maerekebisho

Moja ya Mzee ambaye ni mlemavu wa miguu akitoka Msalani katika eneo la Stendi ya mabasi Simu 2000 ambapo Uongozi wa eneo hilo umeagizwa kutowatoza fedha walemavu

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo (Machi 19, 2017) amezuru na kufanya ukaguzi wa barabara ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura.

Barabara hiyo ambayo ni kiungo kati ya wananchi waendao Sinza, Mpaka Mwenge na Posta hadi Kariakoo sawia na Tegeta hadi Bagamoyo Pwani na Wengine kuelekea Ubungo hadi Morogoro ijulikanayo kama simu 2000 iliyopo katika Kata ya Sinza Manispaa ya Ubungo imeanza kutengamaa kwa gari kupita pasina wasiwasi zaidi ya ilivyokuwa awali.

Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mkururugenzi huyo amesema kuwa Matengenezo hayo yanahusisha kuchonga barabara hiyo, kumwaga kifusi, kumwaga maji na kushindilia ili hata mvua zikinyesha isiathirike na kushindwa kupitika.

"Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imetuamini na kutupa dhamana ya kumsaidia katika majukumu mbalimbali kwahiyo lazima tufanye kazi kwa bidii kwa kufatilia kwa karibu kazi zote tunazoziagiza kwa wakuu wa idara na watumishi wote katika Manispaa ili kuongeza na kukuza ufanisi katika maendeleo ya wananchi" Alisema Kayombo

Kayombo aliongeza kuwa wapo baadhi ya watumishi ambao wanafanya kazi kwa mazoea lakini kwa Manispaa ya Ubungo kumekuwa na utumishi uliotukuka ambapo pia ametumia nafasi hiyo kumpongeza msimamizi Mkuu wa Barabara hiyo sambamba barabara za Manispaa nzima Injinia Goodluck Mbanga kwa ufanisi wa utendaji kazi.

Awali akitoa maelezo ya ukarabati wa barabara hiyo Injinia wa Ujenzi katika Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga alisema kuwa sasa barabara hiyo ipo katika hatua za mwisho za kukamilika ambapo amesema barabara hiyo inaanzia katika makutano ya barabara ya Sam Nujoma na kuishia makutano ya barabaraba ya Shekilango.

Injinia Mbanga amebainisha kuwa Matengenezo hayo ya kiwango cha kawaida ni kwa ajili ya muda mfupi huku Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa katika mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ujenzi wa muda mrefu (DMDP) kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake utaanza haraka Mara baada ya mkandarasi kupatikana.

Sambamba na hayo pia MD Kayombo amemuagiza Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Mabasi cha simu 2000 kutowatoza malipo yoyote wananchi ambao ni walemavu wanaozuru kwenye maliwato iliyopo kituoni hapo.

Naye Msimamizi mkuu wa Kituo cha Siku 2000 Ndg Bakari Shehoza amepongeza agizo hilo na kuahidi kulitekeleza kwa asilimia mia moja kwani limezingatia utu na uzalendo kwa wananchi wote ambao ni walemavu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...