Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
Baadhi ya maofisa wa TBA wakiwa kwenye mkutano na
wajumbe wa kamati hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi wa Bunju B
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B
Mwonekano wa nyumba hizo.Picha na Dotto Mwaibale
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma (PAC) imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumbaza watumishi zilizojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) .
Kamati hiyo imeitaka TBA kuendelea kubuni miradi ya nyumba kwa gharama nafuu ili watumishi waweze kupata nyumba hizo kutokana na viwango vyao.
Akizungumza wa wakati wa Kutembelea miradi ya TBA Bunju B, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Joseph Kasunga, amesema kuwa mradi ni ya gharama kubwa.
Kamati hiyo imesema TBA wamefanya kazi katika kufanya utatuzi wa nyumba kwa watumishi wa serikali wanavyostaafu wanakuwa na makazi bora.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA , Arch , Elius Mwakalinga amesema kuwa wanaendelea kufanya ujenzi katika kuhakikisha kila mtumishi anaweza kupata makazi bora .
Amesema kuwa changamoto za baadhi ya viwanja walinunua na muda lakini kuna watu wanakaa ambapo wameweza kukaa nao jinsi ya kusaidiana
No comments:
Post a Comment