Monday, March 20, 2017

RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. JIM YONG KIM AWASILI NCHINI, APOKEWA NA DKT. PHILIP MPANGO

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akipeana Mkono na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akimuongoza  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim (kulia) kwenda katika eneo aliloandaliwa ili kufanya mazungumzo mafupi  baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt.Jim Yong Kim (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa kwenye mazungumzo mafupi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa kwenye mazungumzo mafupi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), na maafisa wengine wa Serikali walipo wasili katika moja ya Hotel jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)


Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, tarehe 19 hadi 21 Machi 2017. 

Dkt. Kim, akiwa mwenye furaha na bashasha, aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa tano kasorobo usiku na kulakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. DKT. Philip Mpango (Mb), pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo.

Taarifa zilizipo zinaonesha kuwa akiwa hapa nchini, Dkt. Kim atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu, tarehe 20 Machi 2017 ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia utekelezaji wa miradi mikubwa inayo fadhiliwa na Benki hiyo pamoja na kushiriki uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara za Juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange). 

Baadae, Rais Magufuli na mgeni wake watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba mitatu: (i) Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa DART pamoja na ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Ubungo (Dar es Salaam Urban Transport Project (DUTP); (ii) Awamu ya pili ya mradi wa Uboreshaji wa Upatikanaji wa Maji safi na uboreshaji wa miundombinu ya maji taka (Water and Sanitation Project) na (iii) Uboreshaji wa Miundombinu na Huduma za msingi katika baadhi ya miji (Tanzania Strategic Cities Project). 

Miongoni mwa miradi itakayo tembelewa na kiongozi huyo wa juu kabisa wa Benki ya Dunia Dkt. Kim, ni shule ya Msingi Zanaki ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha elimu ya msingi unaogharamiwa na Benki ya Dunia. 

Ziara ya Dkt. Kim imekuja majuma kadhaa baada ya Makamu wake wa Rais anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop alipofanya ziara yake mwezi Januari 2017 ambapo alishiriki uzinduzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi (BRT) uliofanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi hayo kilichopo Kariakoo jijini Dar Es Salaam. 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Fedha na Mipango
Dar es Salaam, 19 Machi, 2017.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Mshauri Mwandamizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia nchi 21 Kanda ya Afrika Bw. Wilson Toninga Banda, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akipeana Mkono na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bi. Bella Bird, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bella Bird na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi Bw. Andrew Bvumbe (katikati) wakifurahia jambo wakati  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim akisubiriwa kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...