Wednesday, March 15, 2017

FEDHA YA UBORESHAJI WA MIJI ZINATAKIWA KUSIMAMIWA KWA UMAKINI –JAFFO

.
.Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akizungumza na watendaji wa Manispaa ya Temeke pamoja na wakandarasi wa mradi wa uboreshaji miji DMDP la Tuangoma leo alipofanya ziara katika maradi huo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
.Mkuu wa Wilaya ya Temeke , Felix Lyaniva akimpa maelezo Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo juu ya mradi wa Mji wa Temeke katika eneo la Tuangoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa manispaa ya Temeke na wakandarasi wa mradi DMDP.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha pamoja na wakandarasi wa mradi wa DMDP leo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Muonekano wa mradi katika mji waTuangoma leo
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo amesema kuwa fedha zinazotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa miji zinatakiwa kusimamiwa kwa umakini.

Jaffo ameyasema hayo leo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja katika eneo la Tuangoma jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Temeke inakwenda kwa kasi katika utekelezaji wa mradi uboreshaji wa miji.

Amesema kuwa baada ya miaka mitano jiji la Dar es Salaam itakuwa imebadilika kutokana na mradi wa uboreshaji miji na kuondokana na mafuriko ya mara kwa mara inayotokana na tatizo la miundombinu.

Jaffo amesema wakandarasi wanaosimamia miradi lazima wafanye kazi kwa kufatilia ili miradi hii iweze kudumu kwa muda mrefu na sio kuwa miradi ambayo baada ya mwaka mmoja kukamilika na kuanza nyufa.

Aliongeza kuwa watu ambao wanatakiwa kufidiwa atafatilia kwa mthamini mkuu wa serikali waweze kufidiwa ili mradi uende kwa kasi na Temeke iwe ya kwanza kuwa mji wa kisasa.

Aidha amesema kwa kutokana na mradi huo uko chini ya ofisi yake atafatilia kwa ukaribu katika kuhakikisha jiji la Dar es Salaam linakuwa na ubora na maji mengine duniani.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...