MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawati kwa viongozi wa kata ya Sao Hill kwa ajili ya matumizi ya shule
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata ya Sao Hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini
Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo, mifungo
10 ya saruji, madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo
10 ya saruji, madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo
Na Fredy Mgunda,Mafinga.
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shuleza msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
Katikaziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia mwenyekiti wake Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo.
Katika hatua nyingine mbunge huyo alitembelea jengo jipya la ukumbi wa kisasa lililojengwa na kikundi cha Agape group ambalo lipo kwenye kata ya Kinyanambo kwa lengo la kuinua kipato cha halmashauri hiyo.
Baada ya mbunge kuona jitihada hizo alichangia 300,000 huku chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ikichangia 100,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo.
Shule ya Msingi Ifungo iliyopo wilayani Mafinga inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ikiwamo Umeme,maji ya bomba, madawati na nyumba za walimu jambo ambalo limedaiwa kuwa kukosekana kwa umeme limesababisha wanafunzi kushindwakufaulu vizuri.
Kilio hicho kimetolewa mwishoni mwa wiki na walimu mkuu wa shule hiyo Tedy Captein wakati akizungumza mbele ya mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi (CCM) wakati mbunge huyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jimbo hilo.
Mwalimu Captein alisema baada ya rais John Magufuli kutoa elimu bure wanafunzi wameongezeka na hivyo wanahitaji maji safi ya bomba badala ya kuelendelea kutumia maji ya tanki ambayo sio rafiki sana kwa wanafunzi hao.
Hata hivyo kutokana na ongezeko la wanafunzi wananchi wameamua kutumia nguvu kazi yao kwa kujenga jengo la darasa moja pamoja na ofisi ya mwalimu kwa gharama ya sh.Mil. sita hadi kufikia kwenye lenta lakini walishindwa kumalizia.
Akijibu kilio cha shule hiyo kuhusu umeme mbunge Chumi alianza kwa kusema“Tutazungumza na shirika la umeme tanesco ili waweze kutuletea umeme ambao utasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule hii.”alisema Chumi.
No comments:
Post a Comment