Wednesday, March 02, 2016

WAZIRI LUKUVI ATEMBELEA KUNAKOBOMOLEWA GHOROFA JENGO LA GHOROFA 16

Mafundi wakiendelea na bomoa bomoa ya jengo  Jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi, wilayani Ilala linamaliziwa kubomolewa na mafundi wa Kampuni ya Patty Interplan baada ya kupewa kazi hiyo na Manispaa ya Ilala ambalo zaidi ya robo tatu ya jengo limeshabomolewa kwani hivi sasa takribani ghorofa 10 zimeondoka.
Mafundi wakiendelea na bomoa bomoa ya jengo hilo ambalo zaidi ya robo tatu ya jengo limeshabomolewa kwani hivi sasa takribani ghorofa 10 zimeondoka.
Waziri Lukuvi akizungumza na baadhi ya watendaji wa mkandarasi pamoja na Halmashauri katika eneo kunakoendelea ubomoaji huo.
Waziri Lukuvi akizungumza na baadhi ya watendaji wa mkandarasi pamoja na Halmashauri katika eneo kunakoendelea ubomoaji huo.
Waziri Lukuvi akizungumza na baadhi ya watendaji wa mkandarasi pamoja na Halmashauri katika eneo kunakoendelea ubomoaji huo.
 Jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi, wilayani Ilala linamaliziwa kubomolewa na mafundi wa Kampuni ya Patty Interplan lilivyo leo.
 Jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi, wilayani Ilala linamaliziwa kubomolewa na mafundi wa Kampuni ya Patty Interplan lilivyo leo.
Waziri Lukuvi akizungumza na waandishi wa Habari



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi amesifu ubunifu, kasi na weledi wa mdandarasi mzalendo wa Kampuni ya Patty Interplan ambayo imepewa kazi ya kulibomoa  Jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi, wilayani Ilala linamaliziwa kubomolewa na mafundi wa Kampuni ya Patty Interplan baada ya kupewa kazi hiyo na Manispaa ya Ilala kwa kusema wameonyesha utendaji uliotukuka.
Amesema kwa kampuni hiyo kuweza kumudu kutekeleza kazi iliyoyashinda makampuni ya kimataifa ni ujasiri mkubwa ambalo litakuwa fundisho kwa wakandarasi wengine wa ndani kufanya kazi kwa kujituma na kwa weledi na ubunifu mkubwa.
"Kwa hapa mwanzoni kwa shughuli hii imekuwa ngumu kidogo kwenu, lakini huu ndiyo mwanzo tu na ninaamini kadri uendelezaji wa majengo unavyoendelea itakuwa rahisi, chapeni kazi zidisheni ubunifu mtakubalika kote,"alisema.
Jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi, wilayani Ilala linamaliziwa kubomolewa na mafundi wa Kampuni ya Patty Interplan baada ya kupewa kazi hiyo na Manispaa ya Ilala.

Utekelezaji wa ubomoaji wa jengo hilo ulianza Februari Mosi kwa kufikisha vifaa katika eneo na ubomoaji rasmi ukaanza Februari 15 kwa kutumia mafundi wa kawaida vibarua zaidi ya 100 wakitumia nyundo, nondo na vifaa vingine na hivyo kurahisisha ubomoaji na kufunga barabara zinazozunguka jengo hilo.

Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Patty Interplan Bw. Mbena alisema kwamba kazi hiyo iliwawia ngumu mwanzoni wakitumia siku tatu kubomoa gorofa moja lakini kwa sasa angalau wanaweza kbomoa ghorofa moja kwa siku moja.

Mmoja wa mafundi ambaye alikataa kutaja jina kwa kuwa siyo msemaji, alisema ubomoaji wa maghorofa huanzia juu na kuteremka chini. “Kama unavyoona ghorofa ya saba ndiyo tunamalizia kuibomoa, kesho (leo) tutakuwa tumeimaliza na tutaanza kubomoa ghorofa ya 6,” alisema.
Alisema wameanza kubomoa ghorofa ya juu na wataendelea kushuka hadi chini.

Kampuni hiyo ilipewa kazi ya kubomoa jengo hilo kwa gharama ya Sh1 bilioni zitakazolipwa na mmiliki wake, Ali Raza Investment. Serikali iliamua jengo hilo livunjwe baada ya kujengwa chini ya kiwango. Hatua hiyo ilikuja baada ya jengo lake pacha kuanguka na kuua watu 37 na wengine 18 kujeruhiwa.

Baada ya ubomoaji kusuasua, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kubomoa jengo hilo akisema litasababisha maafa.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...