Friday, October 02, 2015

UJENZI WA MSIKITI KIMBANGULILE , MKURANGA PWANI

 Msikiti mpya wa Kitongoji cha Kimbangulile, Mkuranga Pwani
 Msikiti wa zamani wa Kitongoji cha Kimbangulile Wilaya ya Mkuranga mkoni Pwani.
Tunamshukuru Mungu kwa wale wote walio tuunga mkono katika harakati hizi Mungu awabariki.
 
Zaidi pia Mungu awabariki waendeshaji wa blog hii ya Jamii kwa kutuunga mkono katika kupeleka habari kwa Jamii na kutuunga mkono katika harakati zetu.
Ndugu zangu Wapendwa Michango tuliyo kusanya toka mwanzo Program PROJECT zetu za kheri hizi ni Tshs 6,000,000 ( Milioni Sita ) .
Pesa hizi zimetumika katika kuwezesha kufanya Mambo Mawili katika sehemu tofauti , Sehemu ya Kwanza ni Mkoa wa Pwani , Wilaya ya mkuranga , Kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha Kimbangulile hapa tumewezesha kuubadilisha ki ujenzi Msikiti kutoka katika hali ya Nyasi kuwa hali ya bati kama mnavyo ona katika Picha . 
Hii ilikuwa ni Project yetu namba Moja .
Matumizi ya hapo tuliweza nunua Tofali 1500 katika Tofali 2000 zilizo tumika kujenga Jengo jipya.
Pesa yote iliyo baki tuli amishia Project namba mbili ambayo ipo mbezi Salasala ambapo tulinunua pesa zote tofali na wakatokea Wahisani wengine walituongezea Tofali ambazo idadi yake zilifikia 10,000/= pamoja na Mifuko 100 ya Cement .
Kwa Mchango huo tuliweza kufanya yafutayo:-
1.Tumejenga Msikiti ambao mnao uona katika Picha .
2.Madarasa Matatu .
3.fremu 3 . 
Na tofali zimebaki kwa ajili ya kujenga uzio.
Mdau katika kheri kwa Michango yenu ndio tumeweza kufika hapa .
Mungu awabariki zaidi na zaidi ili mpate kulikamilisha hili na mengine ya kheri .
 Project ya pili
Katika Project Site namba mbili tumechimbiwa kisima na Mfadhili , kisima kina Mita 120 ametutaka katika Mita hizo tutoe Tshs Milioni Nne ambapo mpaka sasa nina Tshs 125,000/=
Tunawakaribisha wale wote ambao wapo tayari kuchangia kwa lolote katika harakati hizi za kheri.
 
Mahitajio 
1.bati 
2.mbao
3.Nondo
4.Kifusi 
5.Madirisha na Milango 
6.Na vifaa vyote ambavyo vinaweza kutusaidia katika Mambo ya Ujenzi .
Nawashuru saana na saana kwa kutoa muda wako na kusoma maelezo haya , furaha yetu zaidi itakuwa pale utakapo kuwa na muda na utayari wa kututembelea site ilitupate muongozo zaidi kutoka kwako.
 
NAMBA ZA MAWASILIANO YA KUTUMA MCHANGO.
 
TIGO – PESA 
 
+255715800772 
+255673800772 
AIRTEL – MONEY
+255689604780 
Kwa wale walio nje wanaweza tuma kupitia 
WESTERN UNION :
Receiver Name :- GHALIB NASSOR MONERO.
Tafadhali naomba nijulishe mara tu utakapo tuma Mchango wako au kabla kwa Namba hizo za Simu.
Au face book : Kijana wa Kiislam Dsm .

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...