Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma akitoa heshima zake za mwisho kwa askari wa JKT wa kikosi cha 821 Bulombora Kigoma waliofariki jana kwa ajali ya gati.
Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma wakitoa heshima zao za mwisho kwa askari wa kikosi cha 821 JKT bulombora waliopata ajali ya gari jana na kufariki dunia.
Askari kutoka vikosi na majeshi mbalimbali wakiwa mbele ya majeneza ya askari wenzao wa kikosi cha 821 JKT Bulombora waliofariki jana kwa ajali kwaajili ya kutoa heshima za mwisho.
Askari wa majeshi yote wakishirikuana kuweka miili ya wenzao katika eneo la kutilea heshima za mwisho waliofariki jana kwa ajali ya gari.
Na Editha Karlo,wa Blog ya jamii
MIILI saba ya vijana wa jeshi la kujenga Taifa(JKT) kikosi cha 821 Bulombora waliofariki dunia jana kwa ajali ya gari wameagwa leo na kusafirishwa makwao kwaajili ya mazishi.
Akiongea na waombolezaji waliofika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa kigoma(Maweni)kwaajili ya kuaga miili ya marehemu Mkuu wa vikosi vya Kigoma, Kanali Msuya alisema jeshi limepoteza nguvu kazi ya Taifa .
Alisema mpaka sasa taratibu zote za kusafirisha miili hiyo zimeshakamilika miili yote itaondoka kwa usafiri wa magari hadi mwanza na kesho watasafirishwa na ndege ya jeshi kwenda dar es salaam kwaajili ya kupelekwa kwenye mikoa yao kwa maziko.
Kanali msuya aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MT 54407 SGT Ally Kambangwa mkazi wa mtwara,MT 108151 PTE Abeli Maisha mkazi morogoro,SM Eugini Bitati mkazi wa kibondo.
Wengine ni AH 7190 SM Saidi Sadara mkazi wa Shinyanga,RES Bakari Kibaya mkazi wa Tanga,RES Fredrick Kahemela mkazi wa arusha.
Msuya aliwataja majeruhi pia majina yao kuwa ni Benadicto Ndokeye,Raphael Yohana,Athanas Emanuel,Abuu Nzoge,Abubakari peter,Abubakari Msubi na Denis Manyanya.
Wengine ni Edward Nyanda,Elias Magessa,Gofrey Maliki,King Kasefu,Kamilius Agida,Stive Denis,Saidi Omary,Saidi Zuberi,Shabaani Zakari,victor John,Jackson Nyarubu na Mohamed Nyimbo
Naye katibu tawala wa Mkoa wa kigoma eng.John Ndunguru alisema kuwa serekali ya mkoa imepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya askari hao saba na watashirukuana na wafiwa bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu
"Serekali ya mkoa ina masikitiko makubwa kwa kupokea habari hizi za kuondokewa na askari wetu tutashikiriana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu"alisema Ndunguru.
No comments:
Post a Comment