Sunday, February 28, 2010
Mashujaa Bendi yatikisa Vingunguti
-Neema Mkama Gumzo
-Mashabiki wajimwaga kuselebuka
Bendi mpya ya muziki wa dansi nchini MASHUJAA BAND, juzi iliweza kushambulia jukwaa la ukumbi wa Mashujaa Pub uliopo Vingunguti Dar es Salaam ambapo Wimbo Mpya wa Moshi wa Sigara ulionekana kuwavutia mashabiki walioweza kujitokeza kutokana na kuwagusa wengi hasa mwanamuziki kijana mdogo mwenye kipaji cha hali ya juu PATIENCE NSIMBI (pasia budance) unaongelea mapenzi namna ambavyo yanaweza kutoweka kama moshi wa sigara.
Bendi hiyo ambayo ilikaa kambini kwa zaidi ya siku 40 maeneo ya kigamboni ambako walikamilisha nyimbo mpya 6 ambazo zimeanza kuwa na mguso kwa jamii kutokana jinsi zilivyoimbwa, na hivyo kudhihirisha kwamba kimya walichokuwa wamekiweka kilikuwa na mafanikio.
mkuu wa bendi hiyo ELYSTONE ANGAI ambaye ni mzoefu katika fani ya muziki alizikoga nyoyo za mashabiki mara kwa mara kutokana na uhodari wake wa kulicharaza gitaa la solo huku akisaidiwa na mwanamuziki mkongwe EDWARD ANTONY MALIKIDOGO (jadol feed force), katika kukoleza kutokana na Sauti yake kuwaingia wote walioweza kushuhudia burudani hiyo.
Aidha katika Wimbo wa pili, MWANIKE ulioimbwa kwa mchanganyiko wa lugha 3 yaani Kiswahili,Kisukuma na Kihaya pia ulionyesha kuwavutia wengi walioweza kufika katika ukumbi wa makumbusho ikiwa ni katika onyesho maalum.
“kanda ya ziwa kaeni mkao wa kula” alisema Shaaban Mpalule ambaye ndiye msemaji wa Bendi hiyo, wimbo huo umetungwa na Mwanamuziki na rapper wa bendi SIMON NGOSHA(ngosha masanja)
bendi hiyo inaundwa na Wanamuziki wengi wazoefu na chipukizi jumla wakiwa 25 wakiwemo 7 wenye uraia wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na wengine watanzania ,wamo pia kina dada wanaopamba jukwaa la bendi hiyo,yaani wacheza shoo,idadi yao ni 8 amabao pia ni wazoefu.
“Kazi ndiyo imeanza, ila inaonyesha matumaini makubwa kutokana na kile ilichowapa leo mashabiki waliofika hapa Mashujaa Pub, si tu kwamba nyimbo zimewakoga mashabiki wa Dansi bali pia wacheza shoo wanao mvuto kitu kilichopelekea mashabiki kuwa na hamu ya kutaka kuwaona wakiselebuka, kama ulivyowasikia mashabiki wakimwagia sifa kemukemu mcheza shoo wa kike Neema kutokana na Uhodari wake wa kuzungusha nyonga, ni chipukizi ambaye bila shaka anaweza kuwa tishio katika medani ya muziki wa Dansi ususani katika eneo lake la kujidai(Unenguaji) huyu anafananishwa na nyota wa miondoko hiyo hapa nchini Aisha Madinda”alisema Mpalule.
Na kuwataka mashabiki kujitokeza katika maonyesho yake ili waweze kushuhudia ikiwa ni pamoja na kupata baadhi ya nyimbo zilizokwisharekodiwa, ambazo tayari ziko sokoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment