Tuesday, February 23, 2010

Manowari ya Kivita ya Marekani yazuia shambulizi la kiharamia dhidi ya Meli ya Tanzania




Manowari ya Kivita ya Marekani iitwayo USS Farragut ambayo ilizuia shambulizi la kiharamia lililofanywa dhidi ya Meli ya Kitanzania MV Barakaale 1 hapo Februari 21, na kuwakamata maharamia waliohusika katika tukio hilo. Baada ya kupokea taarifa ya kuomba msaada kutoka kwa Nahodha wa MV Barakaale, Helikopta aina ya SH-60B Seahawk kutoka katika Manowari ya Jeshi la Marekani iitwayo USS Farragut iliwasili na kuzuia mashambulizi mawili dhidi ya meli hiyo ya Tanzania.

*************************************************************************************
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Februari, 23, 2010

Manowari ya Kivita ya Marekani yazuia shambulizi la kiharamia dhidi ya Meli ya Tanzania
Maharamia nane wakamatwa

Hapo tarehe 21 Februari, manowari ya Kivita za Marekani ilizuia shambulizi la kiharamia lililofanywa dhidi ya Meli inayopeperusha bendera ya Tanzania ya MV Barakaale 1, na kuwakamata maharamia waliohusika katika tukio hilo. Baada ya kupokea taarifa ya kuomba msaada kutoka kwa Nahodha wa MV Barakaale, Helikopta aina ya SH-60B Seahawk kutoka katika Manowari ya Jeshi la Marekani iitwayo USS Farragut iliwasili na kuzuia mashambulizi mawili dhidi ya meli hiyo ya Tanzania.

Helikopta hiyo iliweza pia kuwazuia maharamia hao kutoroka kwa kuurushia risasi za onyo mtumbwi wao pale ulipojaribu kuondoka eneo hilo kwa kasi. Hatimaye askari waliokuwa katika USS Farragut waliweza kuingia katika chombo hicho na kuwatia nguvuni washukiwa nane wa uharamia huo. Kwa sasa washukiwa hao wanashikiliwa ndani ya manowari hiyo ya Marekani.

Manowari Farragut ni sehemu ya kikosi maalumu cha kimataifa kijulikanacho kama Combined Task Force 151, kilichoundwa Januari 2009 kwa lengo la kukabiliana na uharamia katika eneo la Ghuba ya Aden na Pwani ya mashariki mwa Somalia, kikiwa na lengo mahsusi la kuzuia, na kupambana na uharamia ili kulinda usalama wa vyombo vya usafirishaji majini na kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinakuwa na uhuru wa kupita katika eneo hilo kwa faida ya nchi zote.

Kikosi hiki maalumu ni sehemu Jeshi la Wanamaji la Kimataifa (The Combined Maritime Forces) linalolinda doria katika eneo la kilomita za mraba milioni 8.6 za bahari ya kimataifa ili kuwa na jitihada na uratibu wa pamoja na hatimaye kufikia lengo la pamoja: kuimarisha usalama na ustawi wa eneo hili.

Jeshi la Wanamaji la Kimataifa linalenga katika kupambana na ugaidi, kuzuia uharamia, kuzuia usafirishaji haramu wa watu na madawa ya kulevya na kuhakikisha mazingira ya bahari yanakuwa salama kwa wasafirishaji wenye biashara halali. Jeshi la Kimataifa la Wanamaji linajumuisha takribani dazani tatu za manowari kutoka nchi za Australia, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Pakistan, Kanada, Denmark, Uturuki, Marekani na Uingereza pamoja na majeshi ya wanamaji kutoka nchi nyingine kadhaa.

Jeshi la Wanamaji la Kimataifa na Kikosi Maalum cha Combined Task Force 151 wamekuwa na mafanikio makubwa katika kuzuia vitendo vya uharamia katika Ghuba ya Aden na Pwani ya Somalia. Japokuwa majaribio ya uharamia yameongezeka katika miaka michache iliyopita, katika kipindi hicho, idadi ya matukio ya uharamia yaliyofanikiwa imepungua kwa asilimia 40.


AMERICAN EMBASSY
686 OLD BAGAMOYO ROAD, MSASANI, P.O. BOX 9123, DAR ES SALAAM, TEL. (255-22) 2668001, FAX 266-8251
HYPERLINK "http://tanzania.usembassy.gov"http://tanzania.usembassy.gov

2 comments:

Anonymous said...

Man acha kuchapia hii sio manoari (Submarine) ndio maana mmechapia mpaka kwenye gazeti hii ni meli ya kijeshi ama melikebu. Acha ufala unakuwa kama mimi!

Anonymous said...

Man acha kuchapia hii sio manoari (Submarine) ndio maana mmechapia mpaka kwenye gazeti hii ni meli ya kijeshi ama melikebu. Acha ufala unakuwa kama mimi!

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...