Wednesday, February 10, 2010

Kikwete mazishini kwa Mnikulu


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa mnikulu marehemu Rajabu Kianda, huko Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro jana mchana.Marehemu Rajabu Kianda alifariki jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya kuugua shinikizo la damu na kupata kiharusi (picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto) akiwa na waumini wengine wakiuombea mwili wa marehemu RaJABU Kianda aliyekuwa mnikulu muda mfupi kabla ya mazishi yake huko Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro jana mchana.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa mnikulu huko Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

WAZIRI MKUU: FEDHA ZA MUUNGANO ZITUMIKE KUKARABATI MIUNDOMBINU YA BARABARA

  WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha ...