Monday, June 16, 2008

Mzee ruksa ashindwa kukwea mlima Kilimanjaro


INAWEZEKANA ushauri wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kumtaka Rais Mstaafu, Alhaji Alli Hassan Mwinyi asifike kileleni umefanyiwa kazi baada ya Rais huyo mstaafu kuishia urefu wa meta 3,000 kutoka usawa wa bahari.

Mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika una urefu wa meta 5,896 na kama Alhaji Mwinyi angefika kileleni basi angweka rekodi ya kuwa kiongozi wa ngazi ya Juu kabisa Serikalini kuwahi kufika kileleni.

Alhaji Mwinyi ambaye alianza safari ya siku sita ya kupanda mlima huo Jumamosi iliyopita saa 3:15 asubuhi kupitia lango kuu la Machame na kufika kituo cha kwanza cha Machame Camp saa 10:00 Jioni.

Hata hivyo, Rais huyo mstaafu hakuendelea kupanda Mlima huo na kurejea juzi saa 4:00 asubuhi na hii imetadsiriwa kuwa huenda alisikiliza wosia wa Waziri Mkuu Pinda wakati akimuaga hiyo juzi.

Meneja uhusiano wa Kampuni ya Geita Gold Mine(GGM), Ahmed Merere alilithibitishia Mwananchi jana kurejea kwa Rais Mstaafu, lakini akasema kurejea kwake si kwamba ameshindwa kuendelea bali ni uamuzi binafsi. Habari hii ya mdau
Daniel Mjema aliyekuwapo Hai, Kilimanjaro.

No comments: