Tuesday, June 10, 2008

Kaseja: Nimefuata maslahi Yanga



KIPA Juma Kaseja amesema amewataka viongozi wa Yanga kukamilisha uhamisho wake kutoka Simba ili aanze kuichezea klabu ambayo amesema ameifuata kutokana na maslahi makubwa, huku akiacha viongozi wa Mtaa wa Msimbazi wakihaha kujaribu kumzuia.
Kaseja, ambaye hakuwemo kwenye orodha ya wachezaji waliokuwa wakiwaniwa na Yanga, alishangaza wengi juzi aliposaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo ya Jangwani licha ya kubakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
''Kabla sijasaini mkataba Yanga, niliwaonyesha mkataba wangu ambao nilisaini Simba lakini viongozi wa Yanga waliniambia nisaini na kwamba watamalizana na viongozi wa Simba,'' alisema Kaseja alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Mzalendo Pub jijini Dar es Salaam.
"Ni viongozi wa Yanga wamenihakikishia kuwa watamalizana na wenzao wa Simba ili niweze kucheza. Hatma yangu sasa iko TFF, iwapo TFF wataniambia nichezee Yanga, nitafanya hivyo na kama wakinizuia, nitarejea Simba.
''Sina ugomvi na viongozi, mashabiki na wadau wa Simba. Bado nina mapenzi na mashabiki na wanachama wa Simba. Lakini hilo halinizuii kucheza sehemu yoyote ambayo nataka. Najua kuwa nitapata taabu katika kipindi hiki, lakini kwa kuwa nimeichezea Simba kwa miaka mitano bila ya matatizo, uamuzi wangu uchukuliwe kama hali ya kawaida ya kiuanamichezo.
Habari na Clara Alphonce

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...