Sunday, June 29, 2008

Kilimanjaro Music Award







WASANII kumi wamechaguliwa kuingia katika shindano la kumsaka Mfalme wa hip hop hapa nchini baada ya mashabiki kupiga kura zao kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Wasanii ambao wamechaguliwa katika shindano hilo ni Kalapina wa kundin la Kikosi cha Mizinga, Chid Benz kutoka La Familia, Fid Q, Kala Jeremiah, Joe Makini, Langa, Lord Eyez kutoka Nako2Nako, Rado, Black Rhino na Profesa Jay maarufu kama Daddy.
Akizungumza na Mwananchi, Mratibu wa Shindano hilo, Charles Mateso alisema lengo la kaunzisha shindano hilo ni kuleta changamoto kwa mashabiki na hata wasanii wenyewe.
"Kilichofanyika tuliendesha zoezi la kuwataka wasomaji wetu wachague ni wasanii gani wanaofaa kuingia katika shindano hilo, ambapo baada ya majumuisho ya kura zote walipatikana wasanii kumi na hao ndiyo watakaoliwania taji hilo," alisema.
Alisema mshindi wa shindano hilo atapatikana kutokana na kura za wasomaji wa ambao ndiyo watakaomchagua yule wanayemuona anafaa kuwa Ijumaa King Of Hip Hop. "Litakuwa ni shindano la wazi na hakuna kumpendelea mtu, ila mashabiki ndiyo watakaoamua nani anastahili."
“Ili kumpata mshindi wasomaji wanatakiwa kupiga kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuandika neno HP (acha nafasi), andika jina la msanii unayeona anastahili kushinda taji hilo na kutuma kwenda namba 15551,” alisema.
Kuhusu zawadi alisema mshindi atapata zawadi kubwa itakayotangazwa hapo baadaye, huku yule aliyeshiriki kupiga kura naye akiwa katika nafasi ya kujishindia zawadi kemkem zilizoandaliwa kwa ajili yao. Picha zote kwa hisani ya mdau wa blogu hii Deus Mhagale ambaye alikuwamo ukumbini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...