Sunday, June 08, 2008

Mrema alazwa KCMC asema ni India ya wanyonge



MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Mrema, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC tangu Jumanne, wiki hii akisumbuliwa na homa ya mapafu.

Huku akiwa amelala kitandani, alisema katika siku chache alizolazwa KCMC kwa ajili ya matibabu amebaini kuwa uongozi mzima wa hospitali ya KCMC, madaktari na wauguzi wanafanya kazi ya kutoa huduma usiku kucha hali ambayo inatakiwa iungwe mkono na serikali.

Mrema akizungumza na Mwandishi wa Mwananchi jana, alionesha kukerwa na tabia ya serikali kuwasafirisha viongozi wake kwenda nje ya nchi hususan India kwa ajili ya matibabu ambayo yangewezekana kutibiwa na Madaktari bingwa wa KCMC au Hospitali nyingine za hapa nchini Habari hizi zimetoka Ally Sonda wa Mwananchi Moshi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...