Friday, June 13, 2008

Mufti apasua jipu



Watu wengine wamesema maneno mabaya na wengine wakatangaza amekatwa mguu, na maneno kibao ya kashfa yamemwagwa dhidi ya Mufti, lakini inshaalah Mwenyezimungu kamjaalia Mufti Issa Bin Shaaban bin Simba ambaye amesema leo alichofanyiwa hospitali nchini India, ni upasuaji mkubwa baada ya mguu wake wa kulia kuoza kutokana na kushambuliwa na bakteria, ambao awali alisema hajui namna walivyoingia mguuni.

Hata hivyo, baadaye alisema ana wasiwasi huenda bakteria hao waliingia kupitia majeraha mengi aliyokuwa nayo mguuni.

"Nimerudi, ni mzima, nina afya njema, nina uwezo wa kula na madaktari wana matumaini," alisema Mufti Simba ambaye alikanusha uvumi kwamba, amekatwa mguu, ingawa hakuuonyesha mguu huo kwa viongozi wala waandishi wa habari waliohudhuria mapokezi hayo ili kuufuta kabisa uvumi huo.


"Nimepewa miezi mitatu ya mapumziko nisifanye kazi ngumu, baadaye nitarudi India," alisema Mufti Simba.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...