Monday, March 31, 2008
maafa mererani
Waziri wa Nishati na Madini ,William Ngeleja akizungumza na maafisa wa kampuni ya Tanzanite One, Zane Swanepoel, yaani umbali wa machimbo haya sio mkubwa nashangaa kwa nini hawajaingia kusaidia watanzania waliopata maafa mpaka wafuatwe na mawaziri. Ndio maana wanaapollo wana hasira nao sana, inabidi wabadilike vinginevyo........!!!!!!!!!
Waziri wa mambo ya Ndani, Lawrence Masha akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tanzanite One, Zane Swaanepoel na afisa toka kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Barrick ili kuanza mikakati ya kuopolewa miili ya wachimbaji wadogo jana Mererani.
Askari wa kikosi cha FFU akiwa anawalinda wachimbaji wadogo ambao walikuwa wanazungumza na mawaziri waliotembelea Mererani kutaza maafa. Hawa jamaa kama wakiletewa ujinga hawasikii vibaya kulianzisha zali.
Saturday, March 29, 2008
Kamati Kuu ya CCM
Friday, March 28, 2008
CCM mambo mazito butiama
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara.
Kikao hicho kimeanza tu muda siyo mrefu baada ya Rais Kikwete kuwa amewasili Butiama tayari kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM .
Kikao cha NEC kinaanza kesho ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji ambako alizaliwa Baba wa Taifa na mwanzalishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais Kikwete aliwasili Butiama kwa barabara akitokea Mwanza ambako ndege yake ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza mapema asubuhi na akaamua kusafiri kwa gari kwenye Musoma.
Mjini Mwanza, mamia ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake, walijitokeza kwa wingi, katika baadhi ya sehemu za jiji hilo mvua ikiwa inanyesha, kumshangilia Rais wakati msafara wake ukikatisha mitaa ya jiji hilo kuelekea Musoma.
Mvua inaendelea
Wednesday, March 26, 2008
Balozi Mahiga
Tuesday, March 25, 2008
Anjouan yatekwa na majeshi
MUTSAMUDU-COMORO
VIKOSI vya Comoro vimekiteka visiwa vya Anjouan baada ya uasi uliodumu mwaka mzima
, taarifa za hivi karibuni zinasema.
Taarifa hizo zinasema kuwa vikosi hivyo vinavyotumwa na Umoja wa Afika vimeuteka mji mkuu wa Anjouan na Uwanja wa Ndege bila ya upinzani mkubwa.
Kuna taarifa za kuwepo kwa milio ya silaha nzito mapema leo asubuhi katika kisiwa cha Anzowani.
Mapema Rais Ahmed Abdallah Mohamed Sambi wa serikali kuu ya visiwa vya Komoro alitoa amri kwa majeshi yake kujumuika na yale ya Umoja wa Afrika kukitwaa kisiwa cha Anjouan kutoka kwa kiongozi muasi Kanali Mohamed Bakary.
Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni jana usiku, Rais Sambi alisema kuwa ametoa ruhusa kwa harakati za kijeshi kukikomboa kisiwa hicho kuanza.
Majeshi ya Umoja wa Afrika yanajumuishwa na askari kutoka Tanzania na Sudan na yamekuwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya uvamizi huo, kazi ambayo Rais Sambi amesema itafanyika katika muda wa saa chache zijazo.
Mapema majeshi hayo ya Umoja wa Afrika na yale ya serikali kuu yalidondosha vijikaratasi katika kisiwa cha Anjouan kuwaonya raia ya kwamba majeshi hayo yataingia katika kisiwa hicho katika saa chache zijazo.
Kanali Bakary kwa upande wake alisisitiza kuwa hatajisalimisha na kwamba majeshi yake yako tayari kupambana na uvamizi wowote ule.
Monday, March 24, 2008
Mama weee Bongo kama America
Magari yakwama Chunya
hongera baba
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na Spika wa Bunge, Samwel Sitta na mkewe Margareth wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 40 ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mbali na kuhudhuriwa na Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi, sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Augustino Ramadhan, Naibu Spika Anna Makinda, Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema, Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Mabalozi pamoja na wabunge. Suala la wanaume kutoa fursa za kujiendeleza kwa wanawake ni mojawapo kati ya masuala makuu ambayo yalijitokeza katika nasaha za wanandoa hao, huku mgeni rasmi akisisitiza juu ya suala la uvumilivu na upendo kuwa ni msingi wa kujenga familia bora. Picha na Jube Tranquilino
Mambo ya Dar es Salaam
Usafiri wa wanafunzi Dar es Salaam
Sunday, March 23, 2008
Kc & Jojo wakiwa Bongo
Wanamuziki kutoka marekani Kci & jojo walifaniikiwa kuwasha moto wa ukweli jana ndani ya jiji la Dar es Salaam kwenye show yao ya kwanza iliyofanyika Hotel Movenpic katika kusherekea sikukuu ya Pasaka na kujaza nyomi la watu si kipolepole,kama muonavyo picha Kci & jojo wakifanya vitu vyao ambapo wanamuziki K-lyn na Nakaaya nao walikuwepo kutoa burudani ya nguvu.katika Onyesho lilodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi TIGO. Picha ya Faraja Jube
Pasaka Njema
Ajali ya treni
Friday, March 21, 2008
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Method Kilaini pamoja na wachungaji, wakiwa wamelala kifudifudi kuashiria moja ya matukio ya kuadhimisha kifo cha Yesu Kristo katika Ibada Maalum ya kitaifa iliyofanyika katika Kanisa la Katoliki Mburahati Parokia ya familia takatifu jijini Dar es Salaam. Picha ya Athumani Hamisi
mapambano Comoro kukomboa Anjouan
Mheshimiwa Richard Nyaulawa
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof David Mwakyusa akimfariji mbunge wa Mbeya Vijijini mheshimiwa Richard Nyaulawa ambaye amelazwa katika hospitali ya Indraprastha Apollo nchini india kwa matibabu ya kansa ya utumbo,wakati Prof Mwakyusa na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein walipofanya ziara katika hospitali ya Apollo leo. Mungu ampe nafuu apate kurejea kuendeleza libeneke katika sekta ya habari. Picha kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Thursday, March 20, 2008
Maulidi njemaaa
Mambo ya Maulidi yalikuwa makubwa imefana katika maeneo mbalimbali ya nchi unaweza kuwaona waumini waliokuwamo Mnazi mmoja Dar es Salaam wakiwamo kina Dk Hussein Mwinyi na wengine wengi Pichani baadhi ya kina mama wa kiislam waliohudhuria Baraza la Maulid lilifanyika jana jijini Tanga wakifuatilia kwa makini shughuli mbalimbali zilizokuwazinaendelea katika Hoteli ya mkonge, picha ya chini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mohamed Abdulaziz akitoa salamu mkoa wa Tanga wakati wa Baraza la Maulid ambalo kitaifa lilifanyika jana mkoani Tanga na Mgeni rasmi
alikuwa Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar Ally Juma Shamhuna. (Picha na Tiganya
Vincent, Tanga na Kassim Mbarouk wa Dar es Salaam)
Wednesday, March 19, 2008
Sala ya kumuombea Waziri wa zamani
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakishiriki katika ibada ya
kumwombea marehemu balozi Charles Kileo aliefariki dunia katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili mwishoni mwa wiki . Ibada hiyo ilifanyika kwenye kanisa la KKKT
la Azania Front jijini Dar es salaam jana. Wengine pichani ni Waziri Mkuu
mstaafu, Edward Lowassa , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe (wapili kushoto) na kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph
Warioba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, March 18, 2008
Waweka kambi porini kumpokea Yesu
*Wadai wanamtarajia kushuka nchini kabla ya Machi 30
*Wauza nyumba, mali na kutelekeza jamaa zao
*Serikali yaingilia kati mchungaji akubali kuvunja kambi
Na Richard Kilumbo, Kyela
WAUMINI wa Kanisa la Wasabato wenye imani kali wilayani hapa, wamekimbia makazi yao na kwenda kuweka kambi porini kwa lengo la kujiandaa kumpokea Yesu.
Waumini hao ambao wengine wemetangaza kuuza nyumba na kuwatelekeza ndugu na jamaa zao waliokuwa wakiishi nao, wanaamini kuwa Yesu anatarajia kushuka nchini kabla ya Machi 30, mwaka huu.
Baadhi ya wanafunzi walioathirika na kukimbiwa kwa ndugu na jamaa zao na kuwaacha wakiteseka kwa kukosa mahitaji muhimu, walilieleza Mwananchi kwamba, waumini hao, walianza kuondoka katika nyumba zao wiki iliyopita baada ya ujio wa Mchungaji mmoja kutoka Musoma mkoani Mara, anayedaiwa kuwa Nabii na kuwahamasisha wafanye maandalizi ya kupokea ujio wa Yesu.
Wanafunzi hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walisema ndugu hao wamekimbia makazi na kubeba magodoro huku wakiwaacha wao katika nyumba zao bila msaada wowote.
Walisema wengine wamekuwa wakitangaza kuuza mali zao na nyumba na kwenda kuishi katika pori kubwa lililopo katika Kijiji cha Tenende, wakiamia mahali hapo ndipo patakatifu, ambako Yesu atawashukia.
Mwandishi wa habari hizi juzi na jana alitembelea katika Kijiji hicho cha Tenende na kufanya mazungumzo na baadhi ya watu wanaoishi maeneo jirani na waumini hao.
Wakazi hao, walimweleza kuwa, wamekuwa wakiwashuhudia waumini hao, wakiishi katika pori hilo huku wakikesha kwa kufanya maombi ya mara kwa mara.
Mmmoja wa wakazi hao, Job Anyengenye, alisema hashangai kutokea kwa hali hiyo hivi sasa kutokana na watu wengi kutafsiri biblia wanavyoweza na kutumia kifungu kimoja kama wanavyotaka na kusababisha upotoshaji mkubwa wa imani miongoni mwa jamii.
Alisema kinachomkera zaidi ni pale anapoona watoto wadogo wakiteseka kwa kukosa masomo na wengine wakijikuta wanakwenda umbali mrefu kufuata shule wanazosoma kutokana na wazazi wao, kuhamia porini.
Mzee wa Kanisa la Sabato lililopo Kijiji cha Tenende, Jerad Jackson, alisema kundi hilo ni la waumini waliojitenga kutoka katika Kanisa mama lililopo mjini.
Alidai kuwa, kanisa hilo, uhusiano kabisa na Kanisa Kuu la Kisabato lenye makao makuu yake, mjini Kyela.
Alisema waumini hao wanaendesha huduma yao kwa kufuata misingi na imani zao, wanazozijua.
Baadhi ya Wasabato, wenye imani kali walipotakiwa kuzungumza juu ya uamuzi wao wa kuimbilia porini, walikana kwa madai kuwa sio wasemaji.
Walisema viongozi wao ambao ndio wazungumzaji hawapo.
Hata hivyo, mmoja wao, alisikika hakisema Yesu hawezi kuja mjini ambako kumekuwa na msongamano mkubwa wa nyumba, nyingi zikiwa zinatumika kwa biashara chafu ambazo ni chukizo kwake.
Alisema ndio maana wameamua kwenda porini ambako ni mahali patakatifu Yesu atakaposhukia.
Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya waumini hao zinaeleza kwamba viongozi wakuu wote waandamizi katika Kanisa hilo, ambao ni wachungaji wamesafiri kwenda katika mikoa ya Lindi, Mtwara Tanga na Morogoro kwa ajili ya kuwahamasisha watu waachane na mambo ya dunia na kuuza kila kitu ili washiriki katika ujio wa Yesu.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mashimba Hussein Mashimba amekiri kupata tetesi juu ya waumini hao kuweka kambi porini.
Alisema Serikali inalifanyia kazi suala hilo ili kujua athari zinazoweza kutokea kufuatia uamuzi huo na kutoa uamuzi baadaye.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Suleiman Kova alikiri kusikia taarifa za waumini hao.
Kova alisema kikao cha Ulinzi na Usalama, imekaa na mchungaji huyo, ambaye amekubali kuwarejesha waumini wote katika makazi yao.
"Tumezipata taarifa za hili kanisa na kikao kilichomalizika muda mfupi uliopita kimeamua kwamba waumini wote waliokimbia makazi yao warejee kwao na yeyote atakayekiuka atashitakiwa, " alionya Kamanda huyo.
Alisema kanisa hilo halina usajili na wala halitambuliki na mamlaka zozote halali nchini, hivyo wamemtaka mchungaji huyo, kufuata sheria za nchi kama zinavyoagizwa na kukubali.
Alisema kitendo cha wao (wachungaji) kukikuka taratibu ni kosa kisheria na linashtakiwa chini ya sheria ya kuwakosesha wanafunzi masomo.

Monday, March 17, 2008
Mufti apelekwa India kutibiwa
Na Mussa Juma, Arusha
HATIMAYE Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaban Simba ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari.
Mufti Simba aliondoka jana majira ya saa 11 jioni Arusha kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi baada ya kulazwa kwa zaidi ya wiki mbili.
Mufti (71) aliondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia Airline na atapowasili Mumbai India, atapokewa na gari maalum la wagonjwa kuelekea Hospitali ya Jaslok and Research Center ya Mumbai kuanza matibabu.
Katika msafara huo, Mufti ambaye hivi sasa hawezi kutembea akisumbuliwa sana na mguu wake wa kulia ambao umevimba, ameongozana na Daktari wake, Dk Peter Mhando na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA) Mkoa wa Arusha, Ally Mzee ambaye pia ni ndugu yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, katika hospitali ya KAM – Medical Center , Mufti Simba alisema anakwenda kupatiwa matibabu zaidi katika hospitali hiyo.
Alisema kwa miaka 21, amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa kisukari na kwamba hali yake, ilikuwa mbaya zaidi baada ya kuvimba mguu wake wa kulia.

Dar es Salam bwana
Ona maisha ya watu yanavyoendelea, hakuna hata pa kujipumzisha na jua, mabati yameondolewa katika kituo hiki cha daladala kila mmoja ni mjanja anakula katika umbali wa kamba yake, maisha ni kutaimiana, inasikitisha unaonaje ewe mbongo mwenzangu. Picha imepigwa na mdau Faraja Jube wa Mwananchi na The Citizen.
Sunday, March 16, 2008
Waziri Mkuu yuko Dodoma
Friday, March 14, 2008
Spika aunda upya kamati za bunge
*Muundo wabadilishwa baadhi zaunganishwa
Na Tausi Mbowe wa Mwananchi
SPIKA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ameteua Kamati Mpya za Bunge na kubadili muundo wa baadhi ya Kamati za awali na kuanzisha kamati mpya.
Katika Muundo huo mpya Spika Sitta ameunganisha baadhi ya Kamati za awali kisha kuanzisha Kamati nyingine mpya nne na kufanya idadi ya Kamati hizo za Bunge sasa kufikia 17 badala ya 13 za awali.
Akizungumza na Mwananchi jana Spika Sitta alisema kuundwa kwa Kamati hizo mpya kunafuatia Kamati za awali kumaliza muda wake. Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge, kamati za Bunge zinatakiwa kufanya kazi kwa miaka miwili na nusu.
Spika Sitta alisema kamati hizo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Kamati zisizo za Kisekta, Kamati za Kisekta na Kamati zinazosimamia masuala ya Taarifa za Ukaguzi.
Kanuni za Bunge zinawataka Wabunge kuchagua kwa kuweka alama kulingana na vipaumbele walivyoona inafaa katika Kamati husika. Hata hivyo jukumu la mwisho la kuwachagua Wabunge hao katika Kamati husika ni la Spika.
Padri Kimaro aachiwa huru
Na Bernard James wa Mwananchi
PADRI Sixtus Kimaro (40), aliyekuwa amefungwa jela miaka 35 mwaka 2005 baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana mwenye umri wa miaka 17, ameachiwa huru jana baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali hatia zote mbili na kifungo.
Akitoa uamuzi huo jana Jaji wa Mahakama Kuu, Robert Makaramba alisema amemwachia huru Padri Kimaro kwa kuwa upande wa Mashitaka haukutoa ushahidi wa uhakika kwa mashtaka anayodaiwa kuyatenda kwa kijana aliyekamatwa akiwa naye katika eneo la Changanyikeni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Pia Jaji Makaramba alifuta amri ya awali iliyotolewa ya Mahakama iliyomtaka Padri huyo alipe faini ya Sh milioni mbili.
Jaji Makaramba alitupilia mbali hatia aliyokutwa nayo ya ulawiti akisema hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba wawili hao walikuwa wakitenda jambo lililodaiwa kutendeka.
Baada ya kutolewa uamuzi huo Padri Kimaro alinyanyua mikono yake juu na macho ikiwa ni ishara ya kumshukuru mungu kwa hatua iliyofikiwa na mahakama.
Padre Kimaro alionekana kububujikwa machozi wakati Jaji akiwa amefikia katikati kusoma hukumu hali iliyomfanya atumie kitambaa kujifuta.
Awali akiwasilisha ushahidi wa mteja wake, Wakili wa Padri Kimaro alisema upande wa mashitaka ulishindwa kuwasilisha ushahidi wa kuridhisha kumuunganisha na makosa aliyodaiwa kukutwa nayo.
Padri huyo alihukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakimkabili ya kulawiti, shambulio la aibu na kumdhalilisha mvulana huyo.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika kosa la kwanza la kulawiti na miaka mitano katika kosa la pili la shambulio la aibu na kumtaka mshitakiwa huyo kumlipa Sh2 milioni mvulana aliyelawitiwa. Adhabu hizo zilikwenda sambamba.
Hatimaye wasafiri reli ya kati waondoka Dodoma
Jackson Odoyo na Kizitto Noya wa Mwananchi
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekubali kuwalipa wafanyakazi wake kima cha chini cha Sh200,000 kwa mwezi baada ya kushinikizwa na serikali na mgomo wa wafanyakazi hao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omary Chambo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa serikali imeamua kuingilia kati suala hilo ili kuwanusuru wasafiri wa gari moshi waliokuwa wamekwama Dodoma na Tabora.
Alisema mgogoro kati ya wafanyakazi hao na uongozi wa TRL ulianza siku tano zilizopita na baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya Chama Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), uongozi wa TRL na serikali.
Alifahamisha kuwa TRL imekubali kuwalipa wafanyakazi hao kwa mujibu wa madai yao kwa kuanzia kima cha Sh160,000 kuanzia mwishoni mwa mwezi na ifikapo Sh200,000 ifikapo Agosti, mwaka huu.
"Mazungumzo yetu na,Trawu, TRL yalidumu kwa siku tatu na Mkurugenzi wa TRL amekubali kuwalipa Sh160,000 kuanzia Machi na ifikapo Agosti mwaka huu ataanza kuwalipa kima kipya cha chini cha Sh200,000 kwa mwezi," alisema Chambo. (Picha zote za Michael Uledi)
Makwini wa Mwananchi
Kikosi Kamili cha makwini wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, inayochapisha magazeti ya Mwananchi, mwanaspoti, Mwananchi Jumapili, The Citizen na Sunday Citizen. Kikosi hiki kikiongozwa na mama lao, Maimuna Kubegeya (Mbele Kushoto) kimefanikiwa kwa mbinde kuingia fainali ya Mashindano ya NSSF.
Thursday, March 13, 2008
vyuo vingine bwana
Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...