Friday, March 14, 2008

Spika aunda upya kamati za bunge


*Muundo wabadilishwa baadhi zaunganishwa

Na Tausi Mbowe wa Mwananchi

SPIKA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ameteua Kamati Mpya za Bunge na kubadili muundo wa baadhi ya Kamati za awali na kuanzisha kamati mpya.

Katika Muundo huo mpya Spika Sitta ameunganisha baadhi ya Kamati za awali kisha kuanzisha Kamati nyingine mpya nne na kufanya idadi ya Kamati hizo za Bunge sasa kufikia 17 badala ya 13 za awali.

Akizungumza na Mwananchi jana Spika Sitta alisema kuundwa kwa Kamati hizo mpya kunafuatia Kamati za awali kumaliza muda wake. Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge, kamati za Bunge zinatakiwa kufanya kazi kwa miaka miwili na nusu.


Spika Sitta alisema kamati hizo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Kamati zisizo za Kisekta, Kamati za Kisekta na Kamati zinazosimamia masuala ya Taarifa za Ukaguzi.
Kanuni za Bunge zinawataka Wabunge kuchagua kwa kuweka alama kulingana na vipaumbele walivyoona inafaa katika Kamati husika. Hata hivyo jukumu la mwisho la kuwachagua Wabunge hao katika Kamati husika ni la Spika.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...