Tuesday, March 25, 2008

Anjouan yatekwa na majeshi


MUTSAMUDU-COMORO

VIKOSI vya Comoro vimekiteka visiwa vya Anjouan baada ya uasi uliodumu mwaka mzima
, taarifa za hivi karibuni zinasema.

Taarifa hizo zinasema kuwa vikosi hivyo vinavyotumwa na Umoja wa Afika vimeuteka mji mkuu wa Anjouan na Uwanja wa Ndege bila ya upinzani mkubwa.

Kuna taarifa za kuwepo kwa milio ya silaha nzito mapema leo asubuhi katika kisiwa cha Anzowani.

Mapema Rais Ahmed Abdallah Mohamed Sambi wa serikali kuu ya visiwa vya Komoro alitoa amri kwa majeshi yake kujumuika na yale ya Umoja wa Afrika kukitwaa kisiwa cha Anjouan kutoka kwa kiongozi muasi Kanali Mohamed Bakary.

Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni jana usiku, Rais Sambi alisema kuwa ametoa ruhusa kwa harakati za kijeshi kukikomboa kisiwa hicho kuanza.

Majeshi ya Umoja wa Afrika yanajumuishwa na askari kutoka Tanzania na Sudan na yamekuwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya uvamizi huo, kazi ambayo Rais Sambi amesema itafanyika katika muda wa saa chache zijazo.

Mapema majeshi hayo ya Umoja wa Afrika na yale ya serikali kuu yalidondosha vijikaratasi katika kisiwa cha Anjouan kuwaonya raia ya kwamba majeshi hayo yataingia katika kisiwa hicho katika saa chache zijazo.

Kanali Bakary kwa upande wake alisisitiza kuwa hatajisalimisha na kwamba majeshi yake yako tayari kupambana na uvamizi wowote ule.

1 comment:

Anonymous said...

Your blog keeps getting better and better! Your older articles are not as good as newer ones you have a lot more creativity and originality now keep it up!

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...