Tuesday, March 11, 2008

Bomoa bomoa ya Tabata





Mdau Mpoki Bukuku amepiga picha hizi kutoka Tabata Dampo ambapo nyumba 96 Manispaa ya ilala ilibomoa nyumba zaidi ya 96 hivi karibuni kwa madai kuwa walijenga kinyume na sheria ,wakati hali hii ikiendelea kuwa mbaya siku hadi siku na kusababisha watoto na familia karibu zote kulala kwenye mahema kama muonavyo pichani Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw John Lubuva ameunda tume yenye watu tisa kuchunguza ubomoaji wa nyumba hizo na imetakiwa kufanya kazi yake ndani ya wiki moja. halafu itoe taarifa kwa Halmashari kwa ajili ya utekelezaji wa hatua itakayofuata. picha nyingine Wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) jijini Dar es Salaam wakigawa Sufuria,mablangeti ,na mahema kwa familia za watu waliobomolewa nyumba zao maeneo ya tabata dampo jijini Dar es salaam leo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...