Thursday, September 27, 2007

Makamanda Waula

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo Maafisa wa jeshi la Polisi katika ngazi za Manaibu Kamishna na Makamishna Wasaidizi Waandamizi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Essaka Mugassa, rais amewapandisha vyeo Makamishna Wasaidizi Waandamizi Peter Kivuyo wa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es salaam, Nestory Mpembela ambaye ni Mkuu wa
Idara ya Mawasiliano Makao Makuu na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Omary Rashid Mganga kuwa Manaibu Kamishna.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama amewapandisha vyeo Makamishna Wasaidizi kumi na nane kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi Ambao ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara , Luther Mbutu; Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja , Mselemu Masud Mtulia; Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Zelothe Stephen; na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Seleman Hussein Kova.

Wengine ni Antony Joel Mwami ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Polisi Anga; Neven
Isaack Mashayo Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar; Juma Omary Kondia ambaye ni mkuu
wa mawasiliano Kanda Maalum ya Dar es Salaam; pamoja na Bw Kenneth Kasseke na
Faraji Kayuga wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar

Waliopanda vyeo na kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wengine ni Mkuu wa
Mawasiliano Msaidizi Makao Makuu Abdul Issa Nina; Mkuu wa kitengo cha Maendeleo
cha Jeshi la Polisi Zuhura Munisi, Boniface Kanyunya Mpaze na John Kimario wa
Makao Makuu ya upelelezi Dsm.

Wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi Dsm ambao ni Alexander Calist Mushi, Bw.
Rashid Ally Omar, Bw, Aswegen Wilson Magambo Bw Issaya Juma Mngulu na Mkuu wa
kikosi cha Bendi Makao Makuu, Mbazi Yohana Mchomvu. Mheshimiwa Rais amewapandisha vyeo maafisa hawa wa Jeshi la Polisi kuanzia Agosti 31, 2007

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...