Monday, September 24, 2007

Hasara Sea Cliff zaidi ya Sh 32 bilioni






*Dk Shein atembelea kuona athari
*Asema moto huo umeathiri sekta ya uwekezaji
*Ataka watanzania kuishi kwa tahadhari

Na Kizitto Noya wa Mwananchi

MKURUGENZI Mtendaji wa Hoteli ya Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam, Ketan Patal, amesema hasara iliyosababishwa na kuungua kwa hoteli hiyo ni sawa na thamani ya uwekezaji wa mradi huo aambayo ni zaidi ya Sh32.5 bilioni.

Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Shein aliyetembelea eneo la tukio kuona athari za moto ulioteketeza hoteli hiyo, Patal alisema hata hivyo thamani ya vitu vyote vilivyoungua haijajulikana.

"Haiwezekani kukisia gharama za uharibifu huo sasa, lakini ninachoweza kusema ni kwamba kilichoharibika ni mradi ulioanzishwa miaka kumi na moja iliyopita kwa thamani ya dola za Marekani 25 milioni (sawa na Sh32.5 bilioni)," alisema Patal.

Alisema kwa sasa uongozi wa hoteli hiyo kwa kushirikiana na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, wanachunguza chanzo cha moto huo mkubwa na kutathmini gharama halisi ya uhalibifu uliotokea.

Awali, Meneja Mkuu wa hoteli hiyo, Keven Stander, alimweleza Makamu wa Rais kuwa uchunguzi umebaini kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ingawa hasara iliyopatikana ni kubwa.

Alisema karibu wageni wote waliokuwapo hotelini hapo juzi walifanikiwa kutoka wakiwa salama huku raia wa Uingereza na Ufaransa wakiwa wamechukuliwa na maafisa wa balozi zao na kupelekwa katika hoteli ya MovenPick ya jijini Dar e Salaam.

1 comment:

Anonymous said...

I was very happy to find this site. I wanted to thank you for your time for this fantastic read!

! I definitely really liked every part of
it and I have you saved as a favorite to check out new information
in your web site.

Take a look at my web site how to get followers on instagram

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...