Saturday, September 29, 2007
Zee Comedy hawa aaaa
Hivi kwa mfano hivi sasa liserekali lote la CCM likiwa na baraza la mawaziri 62 limeshindwa kukabiliana na tuhuma za ufisadi alizozitoa mtu mmoja, Dk Willibrod Slaa, pamoja na kujitahidi kufurukuta kujibu, nadhani majibu mmeyaona, kwanza yametolewa kimficho, hakuna aliyejitokeza hadharani akajibu, li-statement limetolewa jioni halafu hakukuwa na mtu, likasokomezwa kwenye vyombo vya habari kiupendeleo, halafu sijui wamepata nini.
Kwanini wasingelitumia kundi la Ze Commedy ambalo leo katika uzinduzi wa mfuko wa uadilifu,uwajibikaji na uwazi (FEAT) katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa rais Dk Mohamed Shein, majamaa wamekamua ile mbaya.
Kwa mfano wangekodi hili kundi likazunguka nchi nzima, pamoja na macommedy lakini mambo yangeeleweka. Angalieni katika uzinduzi wa mfuko huo mambo yalikuwa mukide.
Vyombo hivi ambavyo vinasimama na vinajihusisha na uwajibikaji, uwazi na uadilifu hapa nchini vitapewa uwezo na rasilimali kupitia ufadhili wa mfuko huu vitekeleze kwa ufanisi zaidi majukumu yake ambayo ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya serikali katika azma yake ya kukuza na kudumisha utawala bora.Vile vile mfuko huo utalenga kuvisaidia vyama vya kitaaluma na visivyo vya kiserikali kwa kuvipa uwezo ili kuimarisha maadili ya kitaaluma miongoni mwa wanachama wake.
Aidha baadhi ya asasi/tasisi za umma ambazo zimelengwa kunufaika namfuko huu ni bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na kamati zake,Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, taasisi ya kuzuia nakupambana na rushwa, tume ya haki za binadanu na utawala bora.
Mfuko wa uadilifu,uwajibikaji na uwazi ni sehemu ya mpango huu na umetengewa jumla ya dola za Marekani milioni nne na nusu kwakipindi cha miaka miaka mitano.Mfuko huo utaendeshwa na kamati ya uendeshaji chini ya usimamizi wa sekretari ya maadili ya viongozi wa umma ambayo ni idara inayojitegemea chini ya ofisi ya Rais,utawala bora.Ni hayo tu kwa ufupi washkaji wangu. Picha zimetoka kwa MICHUZI JUNIOR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment