Frederick Katulanda wa Mwananchi anaripoti kuwa madiwani watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejeruhiwa baada ya msafara wa Waziri Mkuu kupata ajali na magari matatu kugongana.
Ajali hiyo imetokea majira majira ya saa 4:45 asubuhi katika barabara ya Nkirizya wakati Waziri Mkuu akitokea uwanja wa ndege kuelekea mjini Nansio.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Zelothe Steven alithibitisha kuwepo kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo ni vumbi.
Magari yaliyogongana ni Toyota Landcruiser STJ 3292 mali ya Tamesa lililokuwa likiendeshwa na Barnabas Dioniz, T 686 ANU mali ya Meneja wa TRA wilayani hapa lililokuwa likiendeshwa na Chacha Kamene pamoja na Toyota Hiace T428 AAD ambalo lilikuwa na madiwani.
Madiwani walioumia na kujeruhiwa ni Juma Mbasa wa kata ya Ilugwa, Bernard Polisi kata wa Kagunguli na Cypriani Nabigambo wa kata ya Bwiro. Madiwani hao wametibiwa na kuendelea na ziara. Chanzo ni vumbi na magari kuwa karibu karibu.
Naye Thobias Mwanakatwe wa PST, Chunya, anaripoti kuwa Msafara wa NaibuWaziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantum Mahiza jana ulipata ajali baada ya gari waliokuwa wakisafiria kugongwa na lori.
Msafari huo ulikuwa na maofisa wa Idara ya Ukaguzi Nyanda za Juu,waandishi wa habari na askari.Ajali hiyo ilitokea juzi 11:45 jioni katika kijiji cha Luwanjilowilayani Chunya Mkoani Mbeya wakati msafara huo ukitokea katika ziaramjini Chunya kurudi Mbeya mjini.
Lori hilo lenye namba za usajili T 683 AFK liligonga gari lenye nambaSTK 3170 ambalo lilikuwa likiongoza msafara wa Naibu Waziri huyo likiendeshwa na dereva Abel Mwakatete likiwa limewabeba maofisa hao.
Maofisa wa Idara ya Ukaguzi waliokuwa katika gari hilo lililogogwa niNaibu Mkaguzi wa Kanda, Mama Arevo, Mkuu wa shule ya Sekondari Tukuyu,Bw. Wakili Mwangoka, mwandishi wa habari wa RTD na mwandishi wa habariwa Kampuni ya The Guardian, Bw. Thobias Mwanakatwe pamoja na askari,Sajenti Seif ambao hata hivyo hawakujeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment