Wednesday, September 05, 2007

Operesheni Okoa Richard

Hi all!



NI wiki ya nne sasa tangu lianze shindano la kumtafunta mshindi wa jumba la Big Brother ambapo tayari washiriki wawili walishatolewa safari hii wanaopigiwa kura ili hatimaye mmoja wao atoke ndani ya jumba hilo ni Meryl, Richard wetu na Maureen. Jamani hebu tuchangamkieni dili tuwapigieni kura hawa wawili Maureen na Meryl, lakini tumpigieni kura nyingi mno Meryl ili Richard na Mareen wabakie.

Ili kupiga kura, tuma ujumbe mfupi wa simu yaani, SMS ukiandika neno VOTE na jina la mshiriki unayetaka aondoke kutoka katika jumba la Big Brother Africa (Mpigie Meryl). Na utume kwenye nambari 15726

Kumbuka kuwa unampigia kura mtu ili atoke ndani ya jumba hilo, kwa hiyo usimpigie kura mshiriki umpendaye. Pia kumbuka kutumia jina la kwanza la mshiriki na siyo majina ya utani wala majina ya wazazi wao.

Pia unaweza kupiga kura kura kupitia tovuti ya www.mnetafrica.com/bigbrother.

Au piga kura kupitia nambari 27-83-900-0000

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...