Waziri wa Nchi, anayeshughulikia Masuala ya Ustawi wa Jamii, Hatua za Kibinadamu na Mshikamano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Eve Masudi ameongoza ujumbe wa DRC kutoa msaada kwa wakimbizi mkoani Kigoma.
Mhe. Masudi amewasili katika kituo cha kupokelea wakimbizi cha ‘National Mills Center’ (NMC), Kigoma na kuukabidhi uongozi wa UNHCR magunia 2000 ya mchele, 2000 ya unga wa mahindi pamoja, magunia ya maharage pamoja na maboksi ya taulo za kina mama ili kuweza kujumuishwa katika mgao wa vyakula vya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. James Millya (Mb.) ameishukuru DRC kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania pamoja na UNHCR katika kuwahudumia wakimbizi hao.
Naye, Mhe. Masudi ametanguliza shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wa kindugu na serikali yake kuwezesha ziara hii ya kwanza na ya kipekee kwao kuja kuwaona ndugu zao.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Bi. Barbara Bentum-Williams Dotse emeeleza furaha yake kufuatia kupokea msaada huo na kushukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa nao bega kwa bega katika kuwahudumia wakimbizi nchini Tanzania, hususani wakati huu ambapo misaada ya kimataifa kwa wakimbizi imepungua kwa kiasi kikubwa.
Hapo jana Januari 14, 2025, Mhe. Masudi alitembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu na kuzungumza na wakimbizi wa DRC kambini hapo.
××××××
.jpeg)



.jpeg)





No comments:
Post a Comment