.jpeg)
.jpeg)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 25 Januari, 2026 ameongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Zanzibar.
Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali ya kimkakati ya Chama na Taifa, ikiwemo kupitisha majina ya wagombea kwa nafasi mbalimbali za uongozi, sambamba na kutathmini utekelezaji wa maamuzi na mwelekeo wa CCM katika kuendelea kuwatumikia wananchi.
Akiongoza kikao hicho, Mhe. Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa mshikamano, uwajibikaji na uongozi makini, akibainisha kuwa maamuzi yanayofanywa yanapaswa kuzingatia maslahi mapana ya wananchi na ustawi wa Taifa.
Kikao hicho kimefanyika Zanzibar, hatua inayoendelea kudhihirisha umuhimu wa Zanzibar katika uongozi wa CCM na uimara wa Muungano wa Tanzania.




.jpeg)



No comments:
Post a Comment