Friday, April 07, 2017

RC GAMBO:WANANCHI LIPENI KODI ZA MAJENGO ILI KUONDOA USUMBUFU UNAOWEZA KUJITOKEZA

Wananchi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kutokana na Sera ya serikali inayisema kila mwananchi inayomraka takiwa kulipa kodi ya majengo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake na kusema kuwa yapo makundi matatu yanayoaanishwa katika ulipwaji wakodi hizo

Hata hivyo amesema makundi hayo ni Pamoja na wale ambao nyumba zao hazijapimwa wala kufanyiwa tathimini,kundi la pili in wale ambao nyumba zao zimepimwa lakini hazijafanyiwa tathimini kundi la mwisho no wale ambao nyumba zao zimepimwa na kufanyiwa tathimini.

Hata hivyo amesema kundi la kwanza linatakiwa kulipa shilingi elfu 15,000kwa mwaka,ambapo kundi la pili wanatakiwa kulipa waendelee kulipa Kwa utaratibu waliokuwa wanautumia toka awali,kundi la tatu gharama zao zipo juu kulingana na tathimini mpya iliyofanyika mwaka 2015-2016.

Vilevile Gambo ametoa onyo kali Kwa wanasiasa wenye tabia ya kupita Kwa wananchi na kuwapotosha kuhusiana na ulipaji wa kodi hiyo amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa endapo watambaini mmoja wapo.

Nae meneja wa TRA mkoa wa Arusha Pili Mbaruku amesema kuwa wamejiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa mitaa ili zoezi la ukusanyaji liwe jepesi kwao badala ya kupanga foleni TRA jambo ambalo litawqchukulia muda wananchi.
Amewataka wananchi kujitokeza Kwa umoja ili kurahisisha zoezi hilo na kuweza kutekeleza agizo la serikali kulipa kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habarimapema  leo ofisini kwake .Picha na Vero Ignatus Blog.

 Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Pili Mbaruku akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa  kwa waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...