Monday, April 03, 2017

MAMA MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA KUMUAGA PAROKO WA KANISA LA MTAKATIFU PETRO FR. STEPHANO KAOMBWE ANAYEHAMIA CHANG'OMBE

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr. Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.

Kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo kipya cha kazi, na pia amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia heri na fanaka kwa uhamisho huo.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr. Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...