Friday, April 21, 2017

PPF YAWATAKA WAAJIRIWA WAPYA KUJIUNGA NA MFUKO WAO

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde akisaini kitabu cha wageni katika banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi baada ya kupata maelezo ya mpango wa ‘ Wote scheme’ ambao umekua msaada katika kuwaongezea mitaji vijana kutokana na mikopo ya mpango huo, waliosimama Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga wakitoa maelezo juu ya huduma za PPF kwa Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati alipotembelea Maonesho ya Mifuko ya uwekezaji kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.
Afisa Mwendeshaji wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati Joyce Rwechungura akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na PPF kwa waliotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inayoendelea katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Kishetu Mhe. Elias Kwandikwa akiuliza swali juu mpango wa ‘Wote scheme’ ulivyofanikiwa kwa watu wote ikiwemo walio kwenye Sekta isiyo rasmi nao kupata nafasi ya kupata mafao mbalimbali. Wanaomfuatilia kwa makini ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Magembe Makoye akimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga kuhusu Mfumo wa ‘Wote scheme’ ambao kima cha chini cha kuchangia ni shilingi elfu ishirini na ndani yake kuna fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.
Michael Silasi (mwenye miwani ) na Said Ally (aliyevaa kofia ) wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel kuhusu kazi za PPF na mafao yanayotolewa na Mfuko huo ikiwemo mfumo wa 'Wote scheme' ambao  utoa fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.


Na Jimmy Mengele - Dodoma. 

 Mfuko wa Pensheni wa PPF unaendelea kuwakumbusha wananchi kujiunga na PPF ili kuweza kufaidika na fursa mbalimbali kama vile mikopo ya maendeleo, elimu, huduma ya afya, mafao ya uzeeni na mafao ya uzazi.

 Akiongea katika Maonesho ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Dodoma, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel alisema hii ni fursa pekee kwa waajiriwa wapya wakiwemo walimu, madaktari na kada zingine kuchagua Mfuko wa Pesheni wa PPF ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kimaendeleo. 

 Afisa huyo alisema waajiriwa hao wapya wakijiunga na PPF watafaidika na mikopo katika maeneo yao ya kazi, mafao ya uzazi, mafao elimu, mafao ya ugonjwa, mafao ya kifo, wategemezi, kiinua mgongo na mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wakati kwa kutumia kikotoo kilichoboreshwa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...