Monday, April 17, 2017

Harmorapa Aandika Historia Mpya Dar Live, Apiga Shoo ya Kibabe

Harmorapa si wa mchezo mchezo! Usiku wa kuamkia leo Ameandika Historia Mpya ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, nazungumzia Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem baada ya kudondosha Bonge la Shoo tofauti n a watu walivyokuwa wakimbeza.Harmorapa ambaye anaonekana kuja kwa speed kali kwenye game ya Bongo Fleva aliisimamisha Dar Live kwa takribani saa 1 kwa kupiga shoo kubwa kwa mara ya kwanza Jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa Ujumla ambapo alikuwa hajawahi kupata nafasi kama hiyo hapo awali.Harmorapa aliwadhihirishia mashabiki wake kuwa yeye siyo wa kubeza kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa wakimfikiria. Ngoma yake ya Kiboko ya Mabishoo ilinyanyua mashabiki wote kwenye viti na kujikuta wakipagawa na kuivamia steji huku kila mmoja akitaka kucheza ngoma hiyo na Rapa huyo. Shoo yake ilikuwa ya kibabe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki waliofurika Ukumbini hapo. Hakika ilikuwa ni Historia kwake na kwa mashabiki wake kumtazama LIVE kwa mara ya kwanza aki-perform jukwaani tena kwenye shoo kubwa kama ile. Katika shoo hiyo, alikuwepo mkali wa Bongo Fleva, Juma Nature, Msaga Sumu na wengine kibao ambao waliangusha burudani ya aina yake ukumbini hapo.
BOFYA PLAY HAPO UCHEKI SHOO NZIMA

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...