Benoit Janin, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel.
· Wateja kuseti simu zao kwenye “automatiki” kuwawezesha kupata mawasiliano ya uhakika mahali popote.
Katika kuhakikisha wateja wake wanapata mawasiliano ya uhakika, Zantel ipo mstari wa mbele katika kufanya maboresho katika mtandao wake ili kuhakikisha kila mmoja anafurahia huduma na bidhaa zao mbalimbali ikiwemo kasi ya mtandao wa 4G.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin anasema, “Tumeendelea kuwekeza katika mtandao wetu kuhakikisha kila mmoja Tanzania anafurahia manufaa ya teknolojia ya simu za mkononi ya Zantel. Uboreshaji huu unaoendelea utaimarisha ubora wa mtandao wetu, kuwa na mtandao ulioenea zaidi kuliko yote hapa nchini na kuwezesha upatikanaji wa intaneti ya kasi kupitia mtandao mpya wa 4G.
Kutokana na mchakato kiufundi kwatika uboreshaji wa mtandao, wateja wa Zantel watahitajika kuhakikisha simu zao zimerekebishwa mpangilio (setting) kuwa atomatik. Zoezi ambalo linaanza sasa mpaka Desemba 31, 2016.
Kwa ajili hiyo tunawaomba wateja wetu kurekebisha simu zao na kuziweka katika sehemu inayoruhusu yenyewe uchaguzi wa mtandao “Automatic Network Selection” kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano ya inteneti ili waendelee kufurahia huduma bora za Zantel.
“Tumejizatiti kuhakikisha mtandao wetu unatoa huduma bora endelevu kwa matarajio ya wateja wetu, wamiliki na wadau wengine muhimu. Kupitia mipango tuliojiwekea, na uwekezaji katika miundo mbinu yetu, tumechukua hatua za makusudi kuhakikisha wateja wetu katika kila kona ya nchi hawachwi nyuma na mageuzi haya ya kiteknolojia”, aliongeza.
Mtandao wa kisasa wa Zantel ulioboreshwa utawawezesha wateja kupata mawasiliano bora na yenye kasi katika upatikaji wa inteneti. Nchi pia itanufaika kwani kasi ya inayopatikana katika mtandao wa 4G itaziwezesha biashara na maendeleo ya teknolojia ya ubunifu na huduma za kidigitali.
Zantel inawakaribisha kila mmoja kujaribu na kufurahia intaneti ya kasi ya 4G.
No comments:
Post a Comment