Wednesday, October 26, 2016

NI KINYUME CHA SHERIA KUMUWEKA MTU NDANI KWA ZAIDI YA MASAA 24

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani linalofanyika mjini Dodoma.

KITENDO cha jeshi la polisi kuwaweka ndani mahabusu zaidi ya saa 24 bila kuwapeleka mahakamani au kuwapa dhamana ni ukiukwaji wa sheria na uvunjifu wa ,katiba ya nchi.Hayo yalisemwana leo Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

“Ni kinyume cha sheria kuweka watu ndani zaidi ya muda uliwekwa kisheria. Lakini watanzania wengi hawajua hili…hii inatokana na uelewa finyu wa naswala ya kisheria,” alisema Mchemgerwa, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo liloandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF).
Alisema wapo watu ambao wanakutana na matatizo mbalimbali pamoja na kuwekwa ndani bila ya makosa kutokana na kutokujua sheria.

Mchengerwa alisema watu wengi hawajui kama kuna dhamana ya polisi ambapo mtuhumiwa hatakiwi kukaa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kupelekwa mahakamani au kupewa dhamana.Katika kongamano hilo,Mchengerwa alisema watoa msaada wa kisheria wanatakiwa kutoa msaada huo katika kila wilaya hususani maeneo ya mjini na vijijini.

"Wapo watu ambao wako gerezani na hawana kosa lakini kutokana na tatizo la uelewa mdogo wa kisheria wamekuwa wakifungwa.
Abdullkarim Saidi, mmoja watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar akizungumza kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wa visiwani Zanzibar.

"Jamii bado haijui kama kuna dhamana ya polisi pia ni kosa la kisheria kumweka mahabusu mtuhumiwa zaidi ya saa24 bila kumpeleka mahakamani au kumpatia dhamana"alieleza.

Aliwataja wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kuwasaidia kuelemisha watanzania kuhusu maswala haya ya kisheria na jinsi ya kupata haki zao pindi wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.

Kwa upande wake mmoja wa watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar, Abdullkarim Saidi alisema licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kutoa msaada wa kisheria, wasaidizi wa kisheria nchini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wasaidizi wa Kisheria walioshiriki kongamano hilo linalomalizika mjini Dodoma leo.

Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosekana kwa usafiri pamoja na fedha za kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, na kuongeza kuwa “tunafanya kazi katika mazingira ambayo si rafiki kutokana na kutembea kwa umbali mrefu.”

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa LSF Bw. Kees Groenendijk amesema shirika lake limeweka mikakati madhubuti ya kuwasaidiza wasaidizi wa kisheria waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kifedha na kitaaluma ili waweze kuwasaidia na kuwafikia watanzania wengi zaidi wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.

Kwa mujibu wa Kees, mpaka sasa shirika la LSF limeshatoa zaidi ya shilingi billion 20 kwa mashirika mbalimbali yanajishughulisha na utoaji wa huduma za kisheria—lengo kuu likiwa ni kuwasaidia watanzania kupata haki zao.

Ramadhani Masele, Progamme Meneja wa LSF, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Wasaidizi wa kisheria wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa uzinduzi wa kongomano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Scholastica Jullu, Programme Meneja wa LSF, akiongea wakati wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria lililofanyika siku mbili mjini Dodoma 25-26, 2016 na kumalizika leo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...