Saturday, October 08, 2016

Mfanyabiashara Dar ajishindia lori la promosheni ya Konyagi

kog1
Mfanyabiashara wa kampuni ya Stewart Jacob Ulomi, Grace Ulomi akiwapungia mkono wafanyabiashara wenzake waliokuwa wakiwani gari lenye thamani ya Sh56 milioni katika mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa na kampuni ya Konyagi, baada ya kuibuka kidedea na kunyakua gari hilo. Mchezo huo uliwashirikisha wafanyabiashara wa Konyagi wapato 25 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Pwani, lilifanyikia Jijini Mbeya.
kog2
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Konyagi, Devis Deogratius (wa pili kutoka kulia) akimpongeza mfanyabiashara wa kampuni ya Stewart Jacob Ulomi, Grace Ulomi baada ya kuibuka mshindi wa gari  lenye thamani ya Sh56 milioni kutoka kampuni ya hiyo katika mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa na kampuni  hiyo.
kog3
Mshindi akifungua mlango wa gari baada ya kukabidhiwa huku akishuhudiwa na maofisa wa TDL 
kog4
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Konyagi, Devis Deogratius (wa pili kutoka kulia) akikabidhi  katoni ya Konyagi mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa na kampuni hiyo
kog5
Baadhi ya washiriki na Maofisa wa TDL wakifuatilia matukio wakati wa droo hiyo
………………………………………………………………..
MFANYABIASHARA kutoka kampuni ya Stewart Jacob Ulomi, Grace Oroki,  mkazi wa Jijini Dar es salaam,   ameibuka mshindi wa gari lenye thamani ya Sh56 milioni katika mchezo wa bahati nasibu ya kwanza ya   promosheni ya nunua ,uza ,shinda na Konyagi  iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya TDL..
Droo ya kwanza ya promosheni hiyo ilifanyika katika viwanja vya hoteli ya  New City Pub jijini Mbeya na ulikuwa na washiriki 25 chini ya usimamizi wa  Ofisa Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya  Taifa ya Michezo ya Kubahatisha , Abdalah  Abeid,na ilikuwa kwa ajili ya mawakala Konyagi kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Pwani.
Akiongea kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Oriki alisema hakutegemea kama angeweza kupata gari hilo kutokana na  ushindani mkubwa uliokuwepo na amepata faraja kwa kuweza kuibuka mshindi.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona.Sikutegemea kuwa nitaibuka na ushindi, ikizingitia awali wote tulikosa ikalazimika kufanya droo mwa mara ya pili na Mola ameniona kuwa mimi ndie mwenye bahati hiyo.  Ni mchezo mzuri uliokuwa wa wazi kabisa. Na gari hili litanisaidia sana kukuza kupato changu katika biashara ya kusambaza bidhaa za  kampuni  ya konyagi kwa wateja wangu,” alisema
Kaimu Meneja     Mkuu wa Konyagi, Devis Deogratius alisema lengo la mchezo huo kwa wateja wake ni kuona anayebahatika anakuwa na uwezo wa kujiongeza katika biashara yake ya usambazaji bidhaa za Konyagi.
 Alisema mchakato wa kuwapata washiriki ulianza Julai mwaka huu  na umechukuwa muda wa miezi mitatu hadi kukamilika na wafanyabiashara (washiriki) waliingia kwenye droo hiyo baada ya kujiridhisha kwamba kila mmoja ametimiza masharti na vigezo vilivyowekwa na kampuni hiyo.
Alisema mbali na mshindi huyo wa gari  katika droo hii ya kwanza washiriki  watano walibahatika kujishindia katoni 10 za Konyagi kila mmoja.
Baadhi ya washiriki katika droo hiyo, Augustine Kisinga na Sebastian Kavishe  walisema wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha droo na wala hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.
Kisinga alisema ‘Kwanza Konyagi kupitia mchezo wa bahati nasibu umetukutanisha na wanafanyabiashara wa maeneo mengine, kwa mfano mimi hapa nilikuwa sijawahi fika Mbeya lakini leo hii nimefika na nimeifahamu Mbeya.
Kwa upande wake, Sebastian Kavishe aliishauri kampuni  hiyo kufanya Promosheni kama hizo mara kwa mara ili kuwapatia motisha wasambazaji wao wakubwa na kuongeza kuwa zawadi kwa washindi  sio  lazima ziwe kubwa kama   gari  bali zinaweza kutolewa zawadi ndogo kama Pikipiki au Bajaj  ili kuwezesha wafanyabiashara wengi kuwa na nafasi ya kushinda na kupata nyenzo za kuwasaidia katika biashara zao.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...