Tuesday, October 18, 2016

DC ILALA AGOMA KUPOKEA RIPOTI YA SOKO LA SAMAKI FERRY

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua sehemu ya soko akiwa ameambatana na Naibu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema akiangalia moja ya Chemba ya maji taka ambayo haina mfuniko wakati kwenye ripoti inaonyesha kuwa chemba hizo zina mifuniko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na mmoja wa wachuuzi wa Samaki katika soko la Samaki Ferry.
Na Humphrey Shao,Dar es Salaam 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, amegoma kupokea ripoti ya soko la Samaki Ferry kutoka kwa Meneja wa soko hilo,baada ya kubainika ''MADUDU'' yaliyomo ndani ya ripoti hiyo.
 
DC Mjema aliamua kufanya hivyo mara baada ya kubaini kuwa makusanyo ya ushuru yaliyomo ndani ya ripoti hiyo ni ya udanganyifu na kwamba mifumo ya uendeshaji iliyopo ndani soko hilo ni dhaifu na haikidhi viwango vya ubora,jambo ambalo linaishushia hadhi soko hilo  ambalo ni maarufu katika  ukanda huu wa Afrika Mashariki na kusini mwa Jangwa la Sahara.
 
"Katika soko hili lazima mmfanye mpango mpya wa kuhakikisha mnaongeza makusanyo ya ushuru kutoka milioni tatu kwa siku na ziadi ili kuhimili huduma zinazohitajika kutolewa kwa wadau wa soko"amesema Mjema.
 
Mjema aliagiza kuwa ndani ya miezi mitatu lazima bodi na uongozi wa Soko hilo kuhakikisha wanajenga matundu ya vyoo Ishirini tofauti na sasa ambapo kuna matundu mawili tu, ambayo yanahudumia watu zaidi ya 4000 katika soko hilo.
Pia aliweka wazi kuwa bodi ya soko hilo ina mzigo mzito wa kuhakikisha soko hilo linarudi katika mstari kama lilivyo kabidhiwa na serikali ya Japan kwa Tanzania.  

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...