Wednesday, October 05, 2016

KAMATI YA MAANDALIZI YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI, YAANZA KUKUTANA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Profesa Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya  mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika  bandari ya  Tanga nchini  Tanzania. Kamati hiyo inajumuishwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya  Fedha, Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG). Lengo la kikao hicho  ni kujadili  maandalizi ya ujenzi wa bomba hilo.
 Mratibu Miradi ya  Ubia wa Sekta Binafsi na Umma (PPP), Salum Mnuna  kutoka  Wizara ya Nishati na Madini (kulia) akielezea maandalizi ya  ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi  Tanzania katika kikao hicho. Kushoto ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara hiyo, Adam Zuberi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa akisikiliza majadiliano yaliyokuwa yanaendelea.
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...