Baada ya Isha kuanza kukamua shabiki huyu alikunwa na hivyo kuvamia jukwaa kwenda kumtunza.
Kabla ya mpambano Abubakari Soud ‘Amigo’ wa Jahazi alipanda jukwaani kuwanogesha mashabiki.
Mtangazaji wa Redio Times FM, Aisha Mbegu (kulia) akirusha sarafu ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kukamua kati ya Leyla na Isha. Kushoto ni mshereheshaji MC wa Jahazi, Mwasity Robert, na katikati ni mwakilishi wa Isha na Leyla.
Sehemu ya umati uliofurika ukumbini hapo kufuatilia mpambano huo.
Leyla akifanya yake baada kupanda jukwaani.
Mtangazaji na MC wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu wa Redio Times FM, uzalendo ulimshinda na kuanza kubanjuka.
Wanenguaji wa Jahazi wakimsindikiza Leyla.
Leyla akiwanogesha mashabiki.
Isha Mashauzi aliyevamia tena jukwaa akiwa katika na vazi jingine.
Isha na kundi lake wakishambulia jukwaa.
Wakati Isha akipagawisha mashabiki, Leyla alikunwa na kumvamia Isha jukwaani na kumtunza hali iliyosababisha mayowe ya kushangilia.
Uhasama wao ulikuwa ni jukwaani tu, kwani baada ya kushuka jukwaani wote walikuwa kitu kimoja.
MASHABIKI wa burudani, hususan muziki wa taarab, usiku wa kuamkia jana walipata burudani ya aina yake wakati wakali wa muziki huo, Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic kwa upande mmoja na Leyla Rashid kwa upande mwingine akiwa na kundi lake la Jahazi Modern Taarab, walipotoana kijasho kwenye onesho maalum la kutaka kujua nani mkali kati yao.
Kabla ya mpambano huo kulikuwa na ubishani mkali kwa mashabiki ambapo upande fulani ulisema Isha ndiye mkali kuliko Leyla huku wengine wakisema “aaah, wapi bwana Leyla ndiyo mkali zaidi; pale Isha haingii hata kwa nini”!
Hatma ya ubishi huo ni mpambano uliowakutanisha wawili hao na kuwaacha mashabiki wakijionea na kuamua wenyewe. Kabla ya wakali hao kupanda jukwaani mshereheshaji wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu, wa Redio Times ilibidi arushe sarafu hewani ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kulivamia jukwaa maana walianza kutegeana. Baada ya sarafu kurushwa Isha ndiye aliyeangukiwa na zali la kuanza kuonesha mavitu vyake jukwaani.
No comments:
Post a Comment