Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akizungumza na Wateja pamoja na Wafanyakazi wa Benki hiyo ikiwa ni muendelezo wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 3 Duniani kote ambapo wateja wa CRDB wataendelea kujivunia mafanikio ya Benki hiyo.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Mohamed Madengelo akizungumza na wateja wa Benki hiyo katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Sherehe hiyo ilipambwa kwa keki.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akishirikiana na mmiliki wa Kampuni ya Easy Connections, Justus Bashara wakati wa hafla hiyo.Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akisaidiana kuandaa vipande vya keki kwa ajili ya wateja na Meneja Mikopo wa benki hiyo, Erick Mgonja.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akimlisha keki mteja wa Benki hiyo, Richard Mlay.
Mmiliki wa Kampuni ya HR Auto Parts Trading, Kisangeta Mihonye akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo.
Wateja wakiwa katika hafla hiyo.
Mmiliki wa Kampuni ya JECEN Building Contractor, Nicholous Mwalituke akitoa shukrani kwa niaba ya wateja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Justus Bashara akishukuru kwa niaba ya Wateja wenzake.
Picha ya pamoja
Tukiwa tunasherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka 2016,tunajivunia kuwa sehemu ya maendeleo na mafanikio yako ya Familia yako,tunaahidi kukupatia suluhisho la masuala ya kibenki ambayo si tu kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara zako, lakini pia kukuhamasisha wewe kufanikiwa zaidi,”ilisema taarifa hiyo.
CRDB iliwashukuru wateja kwa kuichagua Benki ya CRDB na kwamba matumaini yao ni kuendelea kufurahia huduma zao ambazo ni za kibunifu.
“Kwa unyenyekevu na furaha kubwa,kwa niaba ya familia ya Benki ya CRDB nachukua fursa hii kukushukuru kwa kuendelea kutumia huduma zetu, sisi kama Benki tunaamini kwa kiasi kikubwa katika kujenga mahusiano ya kudumu na wateja wetu, siku zote tutaendelea kushirikiana nawe katika kutimiza malengo yako na kufurahia mafanikio tunayopata kwa pamoja".
No comments:
Post a Comment