Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida akiangalia gari jipya aina ya Land Cruiser VXR wakati wa uzinduzi wa jumba la maonyesho ya magari la Kampuni ya Toyota Tanzania jijini Dar es Salaam juzi
Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Mahmood Karimjee wakati wa uzinduzi wa jumba la maonyesho ya magari la kampuni hiyo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kushoto) pamoja na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (kulia) wakifatilia uzinduzi wa jumba jipya la maonyesho ya magari ya Toyota
—
Kampuni ya magari ya Toyota Tanzania Limited imezindua jumba la maonyesho la kisasa kwenye makao makuu yake jijini Dar es salam ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma kwa wateja.
—
Kampuni ya magari ya Toyota Tanzania Limited imezindua jumba la maonyesho la kisasa kwenye makao makuu yake jijini Dar es salam ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma kwa wateja.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Bw. Mahmood Karimjee alisema “Uzinduzi wa jumba hilo la maonyesho unaleta zama mpya katika safari ya Toyota Tanzania, inadhiirisha azma ya Karimjee Group katika kutoa huduma bora kwa wateja. Wateja sasa watafaidika na huduma zilizoboreshwa na bora zaidi kimataifa na tunatarajia watafurahia huduma hii kwa miaka mingi ijayo”.
Jumba hilo kubwa la magari ya Toyota yanayotumika zaidi hapa nchini limeboreshwa kwa kuwekewa huduma nyingi za kisasa kama kumbi za mikutano zenye vifaa vya kisasa ili kuendana na viwango vya kimataifa na litatumika kama maonyesho ya magari ya Toyota hususani aina mpya za magari hayo yakiwemo yale yaliyozinduliwa hivi karibuni kama Hilux pick mpya, Fortuner SUV na Landcruiser VXR.
Kutokana na uwekezaji huu, Toyota Tanzania imelenga kuwapatia huduma mpya na bora wanunuzi wa magari hayo na watu wengine watakaotembelea jumba hilo kujionea huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo. “Kununua gari ni maamuzi muhimu na sio jambo unaloweza kulifanya kila siku. Hivyo basi Toyota imeamua kuhakikisha kila mnunuzi wa gari anaweza kufurahia huduma za kisasa,” alisema Karimjee.
Kufuatia ufunguzi huo, mwakani kampuni hiyo pia itazindua kituo cha huduma baada ya mauzo kwa lengo la kuhakikisha watumiaji wa magari hayo wanaendelea kupata huduma zitakazofanya magari hayo yadumu katika hali nzuri kwa muda mrefu. Vilevile kampuni hiyo itazindua kituo cha kutoa huduma za kuzuia magari yasiharibike na pia itatoa huduma za kukodisha magari kupitia kampuni yake ya Salute Finance Ltd.
Karimjee alisema uzinduzi huu ni historia muhimu katika miaka 191 familia ya Karimjee na miaka 50 ya Toyota hapa nchini kwani jumba la mwisho la maonyesho lilizinduliwa miaka 26 iliyopita.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, mabalozi mbalimbali, wapenzi wa magari ya Toyota na Meneja Mkuu wa Toyota Motor Corporation, Bw. Yu Asano. Ambaye aliipongeza Toyota Tanzania kwa kupiga hatua hii muhimu.
No comments:
Post a Comment